Bi Rehema
mbegu ambae ni katibu wa UVCCM kata ya mwananyamala na kiongozi wa timu ya
garden queen ya kinondoni alitoa vifaa
hivyo baada ya kuombwa kwa muda mrefu na vijana hao ambao yeye pia akiwa kama mlezi wao awasaidie kufanya hivo.
Akizungumza
na wanahabari hizi bi Rehema mbegu alisema
kuwa “kutoa ni moyo na wala si utajiri,niwajibu wetu viongozi kusaidiana katika
sekta mbalimbali, mimi sina uwezo mkubwa
wa kuwatosheleza kwa
kila kifaa cha mazoezi mnachokihitaji ila ninatoa hivi vichache
viwasaidie na kila nipatapo uwezo
sitawaacha nitakuwa nanyi pamoja
kama ilivyo sasa, na wengine
wenye uwezo nimewafungulia njia wajitokezee kuwasaidia mabondia wetu na
ninawaomba wadau wengine wa michezo
,wasiwatenge wanamichezo hasa mabondia, kwani ngumi ni mchezo mgumu na
vifaa
vyake ni ghali mabondia wenyewe hawamudu kutokana na kipato chao
kidogo.hivo tuwasaidie vijana wetu ili tuwaokoe na majaribu ya madawa
ya kulevya na mambo mengine ya kihuni
kama wizi, ukabaji na kadhalika. Nae
kiongozi wa gym ya bigright boxing ya mwananyamal amemshukuru
bi Rehema mbegu kwa msaada wa vifaaa hivyo ambavyo wamesema watavitunza
na kuvitumia vizuri , na tumepata vifaa hivi katika muda muafaka hasa
katika kipindi hiki cha mashindano mfululizo yaliyo mbele yetu, kwa
mfano bondia wetu Issa omari nampepeche atacheza tarehe 29 march na
bondia toka Tanga
zuberi kitandula katika pambano la
raundi sita kuwasindikiza Japhet kaseba
akiminyana na Thomas mashali kugombania ubingwa wa UBO katika ukumbi wa
PTA sabasaba, hivyo vifaa hivi vichache vitatusaidia sana katika mashindano
haya yanayotukabili tufanye vizuri
|
No comments:
Post a Comment