Pages

Saturday, March 22, 2014

YANGA YAONDOA JINAMIZI LA SARE KWA MAAFANDE

                                
Timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, leo imezindukia mjini Tabora na kubadili matokeo ya sare mbili

 zilizopita ambapo leo imeibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Maafande wa Rhino Rangers, mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.


Mabao ya Yanga yalifungwa na Jerry Tegete katika dakika ya 26, kwa shuti kali baada ya mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Mrisho Ngassa, bao la pili lilifungwa katika dakika ya 78, kwa Rhino kujifunga wenyewe kufuatia mpira wa krosi uliopigwa na Simon Msuva. Bao la tatu lilifungwa na Hussein Javu, katika dakika ya 90 aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Jerry Tegete. Hadi mwisho wa mchezo huo Yanga 3 Rhino 0


  



MATOKEO MENGINE 
JKT Ruvu 0 Mbeya City 2

No comments:

Post a Comment