Pages

Monday, April 7, 2014

KIMENUKA: CHADEMA WAMSIMAMISHA MWENYEKITI WA CHAMA HICHO MKOA WA KATAVI




WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chadema mkoani Katavi wameridhia kwa kauli moja na kubariki uamuzi wa kumsimamisha uongozi Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama hicho, John Malack na viongozi wengine watatu waandamizi wa chama hicho, Jimbo la Mpanda Mjini.
Viongozi hao watatu ni pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho Jimbo la Mpanda Mjini, Seif Sipia, Katibu wa jimbo hilo, Joseph Mona ambaye pia ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini kwa tiketi ya chama hicho, Said Alfi.

Katika orodha hiyo yupo pia Katibu Mwenezi wa chama hicho, Godfrey Maufi ambaye ameshavuliwa uanachama wa chama hicho akidaiwa kuiba nyaraka za siri za chama hicho na kuzisoma katika mkutano wa hadhara.

Pia mkutano huo umependekeza kuvuliwa uanachama wa chama hicho watu kadhaa akiwemo Iddi Nziguye ambaye ni Diwani kwa tiketi ya chama hicho Kata ya Makanyagio na Diwani wa Kata ya Kashaulili, John Matongo.

No comments:

Post a Comment