Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA toka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Emmanuel Mahinga akitoa maelezo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam (hawapo pichani) kuhusu jinsi Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma (EPICOR 9.05) unavyofanya kazi na malengo ya kuanzishwa kwa mfumo huo ikiwemo kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo hapa nchini.
Afisa Msimamizi wa Fedha (TEHAMA) toka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Elisa Rwamiago (katikati)akifafanua kwa waaandishi wa habari jinsi Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma (EPICOR 9.) utakavyoongeza tija katika utendaji wa Serikali za Mitaa na kuondoa malalamiko ya kuwepo mianya ya vitendo vya ubadhilifu wa fedha za umma.kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bi Rebecca Kwandu.kulia, ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi Georgina Misama.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bi Rebecca Kwandu (kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es salaam kuhusu faida za matumizi ya Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma (EPICOR 9.05) Katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo Halmashauri 133 na Mkoa 21 ya Tanzania Bara imeunganishawa katika mfumo huo, katikatika ni Afisa Msimamizi wa Fedha (TEHAMA) toka TAMISEMI Bw. Elisa Rwamiago na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi Georgina Misama.
No comments:
Post a Comment