Pages

Tuesday, April 8, 2014

WASANII WAOMBWA KUPEPERUSHA VYEMA BENDERA YA TAIFA ANGA ZA KIMATAIFA

            01
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao cha wadau wa filamu kuhusu mstakabali wa soko la filamu nchini leo jijini Dar es salaam.
02
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini Bi Joyce Fisoo akieleza lengo la kikao cha wadau wa filamu ni pamoja na kujadili masuala ya maendeleo ya tasnia ya filamu nchini na mapendekezo ya wadau kuhusu bodi ya filamu kuitisha mjadala wa wazi wa wadau wa filamu hususani wasambazaji, waandishi wa miswada na watayarishaji ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu tasnia hiyo leo jijini Dar es salaam.
03
Baadhi ya wadau wa filamu walioshiriki kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya husuyo tasnia hiyo leo jijini Dar es salaam. Pichani ni wasanii wa “Bongo Movie” (wa kwanza kushoto ni Steven Mengele “Manyerere”, Emmanuel Muyamba (katikati) na Jacobo Steven “JB”(wa kwanza kulia) 
04
Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (wa sita kutoka kushoto mstari wa mbele) baada ya ufunguzi wa kikao cha wadau wa filamu kuhusu mstakabali wa soko la filamu nchini leo jijini Dar es salaam.

                                                     Picha na Eleuteri Mangi

No comments:

Post a Comment