Pages

Saturday, March 22, 2014

JUMAMOSI TAMU KWA WANAOWANIA UBINGWA WAANGUSHA DOZI NZITO KWA WAPINZANI

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay, Luis Suarez amepiga hat trick timu yake Liverpool ikiifunga mabao 6-3 Cardiff City
katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni. Cardiff walitangulia kupata bao dakika ya tisa mfungaji Mutch kwa pasi ya Campbell, lakini Luis Suarez akaisawazishia Liverpool dakika ya 16 kwa pasi ya Johnson.
Campbell aliifungia bao la pili Cardiff dakika ya 25 pasi ya Mutch na Martin Skrtel akaifungia Liverpool mara mbili mfululizo dakika ya 41 na 54, mabao yote pasi za Philippe Coutinho kabla ya Suarez kufunga la nne dakika ya 60 akimalizia pasi ya Daniel Sturridge.
Sturridge alifunga bao la tano dakika ya 75 kwa pasi ya Suarez kabla ya Mutch kuifungia Cardiff la tatu dakika ya 88, pasi ya Jones. Suarez alikamilisha hat trick yake dakika ya sita ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida kwa bao la sita akimalizaia pasi ya Skrtel. Liverpool sasa inatimiza pointi 65 baada ya mechi 30 na kushika nafasi ya pili katika msimamo.

                    


Wakati huo huo Man City imeifumua Fulham mabao 5-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Etihad. Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure leo amepiga hat trick yake ya kwanza, mabao mawili akifunga kwa penalti dakika ya 26 na 54 na linguine dakika ya 65 akimalizia pasi ya Samir Nasri.
Mabao mengine ya Man City yamefungwa na Fernandinho dakika ya 84, akimalizia pasi ya Milner na Demichelis dakika ya 88. Ushindi huo, unaifanya City ifikishe pointi 63 baada ya kucheza mechi 28 na kupanda nafasi ya tatu mbele ya Arsenal yenye pointi 62 za mechi 30.

                      

 MATOKEO YA MECHI NYINGINE:
Everton 3   Swansea City 2
Hull City 2   West Bromwich 0
Newcastle United 1   crystal Palace 0
Norwich City 2   Sunderland 
West Ham United 0   Man United 2

No comments:

Post a Comment