Pages

Saturday, March 22, 2014

MSAADA: TBL YATOA KISIMA WILAYANI TUNDUMA


                          
Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiud Saideya akiwa na Meneja Matukio Kampuni ya Bia Tanzania TBL Kanda ya nyanda za juu kusini Claud Chawene wakikata utepe kwa pamoja kuzindua kisima hicho cha Maji



                     
Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiud Saideya akiongea na wafanyakazi wakituo cha Afya Tunduma mara baada ya kukabidhiwa kisima hicho na TBL



                      
Afisa uhusiano wa Kampuni hiyo Doris Malulu amesema kampuni ya Bia ni moja kati ya Makampuni yanayoongoza kulipa kodi nchini na hivyo ina wajibu wa kurudisha fadhila kwa Watanzania.




                      
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji mdogo wa Tunduma Elias Cheyo akitoa neno la shukrani kwa TBL



                         
Baadhi ya wafanyakazi na wananchi wa mji wa Tunduma wakimsikiliza mgeni rasmi



                      
Diwani wa kata ya Tunduma Frank Mwakajoka akiwashukuru kampuni ya Bia TBL kwa msaada wa kisima hicho



                               
Afisa mipango Mji wa Tunduma Augustino Ngetwa akisoma taarifa fupi mbele ya mgeni rasmi




                         
Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiud Saideya akiwa na Meneja Matukio Kampuni ya Bia Tanzania TBL Kanda ya nyanda za juu kusini Claud Chawene wakielekea eneo la makabidhiano ya kisima hicho




                                   
Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiud Saideya wakipeana mikono Meneja Matukio Kampuni ya Bia Tanzania TBL Kanda ya nyanda za juu kusini Claud kuashiria kukabidhiwa kwa kisima hicho



                         
Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga wakipongezana na mwenyekiti wa Halmashauri ya mji mdogo wa Tunduma Elias Cheyo mara baada ya kukabidhiwa kisima hicho





                          
                                                  Kituo cha Afya Tunduma


Kampuni ya Bia Tanzania imetoa msada wa kisima cha maji kwa ajili kituo cha Afya Tunduma chenye thamani ya shilingi milioni 24 chenye uwezo wa kutoa lita 5000 kwa saa.
Afisa uhusiano wa Kampuni hiyo Doris Malulu amesema kampuni ya Bia ni moja kati ya Makampuni yanayoongoza kulipa kodi nchini na hivyo ina wajibu wa kurudisha fadhila kwa Watanzania. Malulu amesema kampuni yake imetenga jumla ya shilingi milioni 450 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo nchini kwa kipindi cha mwaka wa fedha yenye nia ya kuisaidia serikali kukabiliana na changamoto mbalimbali.
 

Naye Afisa mipango Mji wa Tunduma Augustino Ngetwa amesema mradi huo utasaidia kumaliza tatizo la maji hivyo kuwa faraja kwa wagonjwa wanaotumia kituo hicho ikiwa ni pamoja na raia wa nchi jirani ya Zambia. Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiud Saideya amesema kuwa watahakikisha wanautunza mradi huo ili uwe na manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho .

Aidha Diwani wa kata ya Tunduma Frank Mwakajoka ameshukuru Kampuni hiyo kwa kutoa mradi huo na hivyo kuwataka wahudumu kuitunza miundo mbinu ya maji. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji mdogo wa Tunduma Elias Cheyo ameitaka kampuni ya bia kupanua wigo wa kusaidia Nyanja nyingine kama vile elimu ili kufanya mji wa Tunduma kuwa na maendeleo zaidi.

No comments:

Post a Comment