kuweza kupata bao la kwanza kwa njia ya penati, baada van Persie kufanyiwa madhambi eneo la hatari, dakika ya 46 akiifungia tena goli la pili na kufanya matokeo kuwa 2-2 baada ya awali kule Ugiriki. Hakuishia hapo kipindi cha pili walirudi kwa kasi na kuwapelekea kuandika goli la tatu kwa faulo safi. Kwa matokeo hayo Man U imesonga mbele kwa jumla ya magoli 3-2.

TUTA: Jose Holebas akimfanyia madhambi na kupelekea muamuzi kuamuru faulo iliyozaa penati

AJALI KAZINI: Valencia alipata uvimbe juu ya jicho

USHINDI RAHA: Leo na nguvu ya kukimbia ilikuwepo bwana

RAHA: Ferguson akishuhudia ushindi

OYOOOOO WELBACK MALIZIA: Ni shangwe tu baada ya kufunga goli la pili
IMEPITA HIYO: Goli la tatu lileeeeee

AKAAA MWEZANGU SIJISUMBUI: Kipa akiuangalia mpira ukijaa kimiani

MAUMIVU: Misuli noma shujaa akiugulia
Wakati huo huo Borussia Dortmund wamekubali kipigo cha magoli 2-1 dhidi ya Zenit Petersburg nyumbani, lakini kwa matokeo hayo haijawaathiri Wajerumani hao baada ya awali kuwekeza idadi nyingi ya magoli. Mbrazil Hulk alifunga goli zuri la freekick dakika ya 16 ya mchezo lakini mkongwe Kehl akaisawazishia dakika ya 38. Hadi mapumziko timu zilikuwa 1-1 bahati ilikuwa kwa Warusi hao kipindi cha pili baada yakupata goli la pili dakika ya 72 kupitia Rondon. Kwa matokeo hayo Borussia imefuzu kwa jumla ya magoli 5-4.

KITU KINAKUJA: Hulk akinyoosha msuli

WABABE: Mashabiki wa Zenit wakichoma bendera za wapinzani wao pale pale Signal Iduna Park.
No comments:
Post a Comment