Pages

Sunday, April 20, 2014

BREAKING NEWS: MOTO MKUBWA WAIBUKA DODOMA MJINI

                                                    
Moto mkubwa umeibuka ghafla katika jengo lenye frame za  maduka linalotazamana na jengo la Makao Makuu ya CCM Barabara ya Nyerere Square Dodoma Mjini hivi punde!
                                
                                                 Moto huo ukiendelea kuwaka

Mpaka dakika hii timu ya Feel At Homee inaingia mitamboni bado moto huo mkubwa unaendelea kuwaka na hakuna chombo chochote cha zimamoto kilichofika eneo hilo.

Mpaka hivi sasa bado chanzo cha moto huo hakijajulikana na pia bado hakuna taarifa zozote za madhala yaliyosababishwa na moto huo huku jengo hilo likizidi kuteketea

Endelea kuwepo karibu na ukurasa huu kwa taarifa zaidi
>>>

                                 
                          Kama unavyoweza kuona pichani moto huo ukiwa umeshika kasi

No comments:

Post a Comment