Mabao kutoka kwa Puncheon dakika ya 23, Dann dakika ya 49 na Jerome dakika ya 73 yalitosha kuwaangamiza Everton katika uwanja wake wa nyumbani. Wageni wakiwa wanakimbia kushuka daraja na mwenyeji kutafuta nafasi nne za juu hili mwakani acheze Ligi ya Mabingwa, licha ya jitihada na kufanikiwa kupata magoli mawili kupitia Naismith dakika ya 61 na Mirallas dakika ya 86 lakini hayakuweza kuwasaidia kuondoka na alama hata moja.

No comments:
Post a Comment