Klabu ya Chelsea imezidi kusogelea ubingwa baada yakumfunga mpinzani
wake wa jiji magoli 6 kwa 0. Iliwachukuwa dakika 4 tu mashabiki
kuanza kufurahi baada ya Eto'o kutofanya hajizi, Arsenal ikiwa inatafakari goli Chelsea wakabika mpira wa kushtukiza na kumpelekea Schuerrle kufunga la pili dakika 6 ya mchezo. Dakika ya 17 Hazard akaiandikia goli la tatu kwa njia ya penati baada ya Chamberlain kuushika mpira kwa makusudi, lakini mwamuzi aliamua kumtoa Gibbs kutokana na adhabu hiyo ikaqalazimu Arsenal wafanye mabadiliko ya Kumtoa Poldoski, bado dakika 3 kueleka mapumziko Oscar akamalizia pasi safi ya Torres na kuandika bao la 4. Kipindi cha pili Arsenal ilifanya mabadiliko ya kuwatoa Chamberlain nafasi yake ikachukuliwa na Flamini na Koscienlny nafasi yake akaingia Jenkinson, dakika ya 66 Oscar tena akafunga goli la 5 na Salah akaiandika goli la 6 dakika ya71. Kwa matokeo hayo Chelsea imefikisha alama 69, alama 7 nyuma ya anayemfuatia
Msaada
Bado Moja
CHELSEA APAA KILELE AMPIGA ARSENAL 6 KWA O

No comments: