Slider[Style1]
Style2
Style3[OneLeft]
Style3[OneRight]
Style4
Style5
SIMULIZI: JOHNSON NA MARIA
Posted by: Unknown Posted date: 9:30 PM / comment : 0 SIMULIZI
SIMULIZI: JOHNSON NA MARIA
Posted by: Unknown Posted date: 9:30 PM / comment : 0 SIMULIZI
Ilipoishia Maria: " mpenzi jiandae kesho ntakufuata Gengeni kwako tuongozane kuna vitu naenda kukununulia"
SIMULIZI: JOHNSON NA MARIA
Posted by: Unknown Posted date: 9:30 PM / comment : 0 SIMULIZI
SIMULIZI: JOHNSON NA MARIA
Posted by: Unknown Posted date: 9:53 PM / comment : 0 SIMULIZI
Ilipoishia Mzee Joseph akamuambia Maria "Binti umependeza sana we mrembo kweli Johnson anajua kuchagua" Maria akacheka kusikia vile
SIMULIZI: JINI CHEKETU - SEHEMU YA 3
Posted by: Unknown Posted date: 6:19 PM / comment : 0 SIMULIZI

ILIPOISHIA:
“MAMAA.. MAMAAAAAAAAAAAAA….!!!” Kelele zilisikika kutoka ndani alipokuwa Ashura. Mama yake akakurupuka mbio kurudi ndani kujuwa nini kilichomfanya mwanawe kupiga kelele zile
“Vipi?..kuna nini!?..Ashura! Ashuraa!! We Ashura!!!” Aliuliza kwa mshangao na kuita huku akiwa amemshika mabegani na kumtingisha. Lakini masikini Ashura wala hakuonekana kutingishika wala kupepesa macho, badala yake akawa ameganda amebutua macho tu kama mtu aliyekuwa akiona maajabu ya mwisho ya Dunia.
“Ashuraaa!!!” Aliita tena bila mafanikio
ENDELEA:“Ashura vipi kwani mwanangu..?!”
“Mamaa..” Aliita Ashura kwa sauti ya chini “Naomba maji ya kunywa”
Haraka haraka mama yake akaukimbilia mtungi ulipo akachota maji kwa kutumia kata moja ndogo ( Kata ni kifaa kinachotumika kama kikombe kwaajili ya kuchotea maji, hutengenezwa kwa kifuu cha nazi kilichokauka na kukwanguliwa na kusafishwa vizuri kisha kuchomekwa mti mwembamba katikati ndio huwa mshikio wake, mti huu mara nyingi huwa ni mpingo au miti migumu ambayo haina madhala inapoloana na maji )
Kabla hata hajafika mikononi mwake akaivamia kata ile na kuanza kuyafakamia maji kwa fujo kama mtu aliyetoka kufukuliwa kwenye tanuli la moto na sasa alikuwa na kiu ya ajabu
“Niongeze..”
Upesi tena mama yake akaugeukia mtungi na kudidibua tena maji ya kutosha akampelekea. Kama alivyoyapokea mara ya kwanza ndivyo alivyoyapokea tena mara ya pili akayafakamia tena bila kujali mengine yaliyokuwa yakimmwagikia kifuani na kulowesha nguo zake za shule. Mama yake akashangaa sana hali ile, laiti ingekuwa mwanawe yupo kwenye hali ya kawaida basi labda angemuuliza ni chakula gani alichokula mpaka anakunywa maji mengi kiasi kile! Lakini akakumbuka kwamba mwanawe yupo kwenye tatizo na pengine tatizo hilo ndilo linalomfanya anywe maji kiasi kile. Hakutaka kupoteza muda
“unaweza kutembea?”
“Hapana mama nasikia kizunguzungu..”
“Kaa twende!!” Alisema huku akiwa tayari kashageuza mgongo na kuchuchumaa ili mwanawe apande mgongoni
“Vipi tena mbona hivyo?!”
“Mtoto anaumwa..” Alijibu mama Ashura kisha akanyamaza kama mtu aliyekuwa akisubiria swali lingine
“Anaumwa nini?”
“Amekuja anakimbia kutoka shule, anadai kichwa kinamuuma sana, mwili hauna nguvu na anasikia kizunguzungu!”
“Sasa huku mnaenda wapi”?
“Nampeleka kule bondeni kwa Ostaadh Jengo, tena afadhali hata tumekutana..”
“Aaaaggh..! Sasa mke wangu, mtoto anaumwa unampeleka kwa waganga wa kienyeji badala ya kumpeleka hospitali?!”
Alikuwa ni mzee mweusi mwenye urefu na wembamba wa wastani, anaitwa SUED SHAABAN GAMBA. Lakini pale kijijini alikuwa akifahamika zaidi kwa jina la Mzee GAMBA. Huyu ndio baba yake mzazi Ashura na ndiye mume halali wa Bi Amina Mwinyi au Mama Ashura. Mzee Gamba yeye hutoka nyumbani asubuhi na mapema sana mara tu amalizapo swala ya alfajiri, kisha kwenda moja kwa moja mashambani. Mara nyingi akitoka kukagua mashamba na mitego yake hufikia kijiweni kwanza kunywa kahawa na kupiga gumzo na wazee wenzie kisha kupitia msikitini kusali sala ya alasiri halafu ndio hurejea nyumbani mida ya mchana. Wakati huo ndio Mama Ashura naye alikuwa amembeba mwanawe mgongoni wakiwa njiani kuelekea kwa mtaalamu wa jadi, ndipo alipokutana na mumewe akiwa anarudi nyumbani
“Lakini mume wangu huu ugonjwa unavyoonekana sio wa hospitali” Alisema mama Ashura kumwambia mumewe
“ Kwanini usiwe wa hospitali wakati umesema anaumwa na kichwa?! Alihoji Mzee Gamba
“ Amedai wakati anarudi kutoka shule amekutana na bibi mmoja…..
“Aaaaaggh..mke wangu ushaanza na imani zako!..umeshaanza tayari hivyo!!”
Mzee Gamba akamkatisha mkewe kabla hata hajamaliza kusimulia na kuonyesha asivyokubaliana na imani hizo. Siku zote alikuwa hataki kusikia maswala ya mganga wa kienyeji, yeye alikuwa ni muumini mzuri wa dini ya kiislamu mwenye kusali sala tano kila siku iendayo kwa mungu, hivyo hakutaka kabisa imani yake ilale kwa waganga wa kienyeji, kitu kilichokuwa kinafanya wapishane sana na mkewe kila linapoibuka swala kama hilo
“Mzee Gamba lakini ujue wewe hukuwepo nyumbani wakati mtoto anarudi, isitoshe amenisimulia kile kilichomfanya awe katika hali hii..! na mimi kwa jinsi nilivyoongea naye na kumuona hali yake si ya kumpeleka hospitali” Alisema mama Ashura kwa uhakika kujaribu kumshawishi mumewe akubaliane na wazo lake
“Sawa mimi sijakataa maamuzi yako mke wangu, lakini kwanza tumpeleke hospitali, kama huduma ya huko itashindikana basi ndio tumpeleke kwa hao unaowaiita wataalamu wako!”
“Mume wangu, kumbuka hospitali ipo mbali sana! Ni mwendo wa karibu saa nzima kwa miguu, na hapa hatuna usafiri wowote! Unafikiri tutafika saa ngapi? Na kama unavyoona hali ya mtoto hawezi hata kutembea!, unataka tumkose?..enhe? unataka tumkose?!” Hakika uchungu wa mwana aujuae mzazi! Hasa mama ambaye ndiye amebeba ujauzito kwa miezi tisa. Mama Ashura akaonyesha hisia zake juu ya mwanawe kipenzi, akakaza sauti, akaunganisha maneno bila ya kumpa nafasi mumewe. “Acha twende hapo kwa Ostaadh karibu kwanza ampe hata dawa ya kumpoza, kama itakuwa tofauti ndio tufanye mpango wa kutafuta usafiri tumpeleke hospitali”
Maneno ya mkewe yalimchoma moja kwa moja Mzee Gamba. Akamuangalia mwanawe aliyekuwa ananing’inia mgongoni kama kinda la ndege anayehisi baridi kali. Akainua mkono akamgusa kwenye paji la uso, joto kali alilolisikia toka kwenye kichwa cha mwanawe lilimshangaza hata yeye. Akaamini kweli mtoto wao yupo kwenye hali tete
“Ashura mama..!” Aliita kwa unyonge Mzee Gamba. Lakini Ashura hakuitikia, si kwamba alikuwa hataki kuitikia ama anamjeuria baba yake..hapana! bali hali aliyokuwa akiisikia aliona hana nguvu hata ya kuongea. Mzee Gamba akagundua hilo, hivyo hakurudia kumwita tena
***************** ***************** ****************** *************
“Hodiiiiiiiii we mzaramoo!!..unalala tu jua kali lote hili?!” Alisikika Mzee Gamba akiita huku akichombeza kwa utani baada ya kufika kwenye uwanja wa nyumba ya Ostaadh Jengo
Ostaadh Jengo alikuwa ni mtaalamu mwenye kuchanganya tiba za miti shamba na kitabu cha Quraan. Watu wengi walimsifu kwa dawa zake ambazo zilionekana kuwa ni msaada mkubwa kwa watu wa maeneo yale pamoja na jirani. Hakuwa mzee, yeye alikuwa ni kijana wa makamo na alikuwa akiishi peke yake na shughuli zake kubwa zilikuwa ni uganga
“Ahaaaaaaa Shekhe Gambaa huyooo!..Karibu sana bwana, nilale saizi nina raha gani rafiki yangu?!” Alikaribisha kwa uchangamfu mkubwa huku naye akichombeza utani ule. Kama ilivyo kawaida kwa watu wa pwani kupenda sana matani na kutupiana maneno ya hapa na pale pindi wanapokutana.
“Haya kulikoni tena mbona mmebebana mchana mchana?!” Alihoji Ostaadh Jengo baada ya kutoka nje na kumuona mama Ashura akiwa amembeba Ashura ambaye alikuwa amejikunja mgongoni kama sungura
“Ebu piteni ndani kwanza” Alisema Ostaadh Jengo kabla hata hajajibiwa swali lake huku akiwa kashageuka na kutangulia ndani, kwani moja kwa moja alijuwa ujio ule ulikuwa ni wa kiugonjwa. Bila kuongeza neno lolote Mzee Gamba na mkewe wakamfuata kuingia ndani
*************** ******************** *****************
Mama Ashura alitumia kama dakika tatu kuelezea ile hali aliyorudi nayo mwanawe ghafla na pia akamsimulia kuhusu kukutana na yule bibi wakati alipokuwa akirudi nyumbani. Bila ya kupoteza muda Ostaadh akachukuwa kikombe kidogo cha udongo akaenda jikoni akaweka makaa mawili matatu ya moto, akafungua kimfuko chake cha karatasi kilichokuwa kimechomekwa ukutani kwenye fito, akatoa kitu kama chengachenga hivi..akaweka kwenye kile kikombe chenye moto, moshi ukaanza kutoka na harufu ya ubani ikaanza kutawala chumba kile. Kisha akachukua kitabu chake akafunua kurasa aliyokuwa anaijuwa yeye akaanza kusoma polepole kwa umakini mkubwa. Muda wote huo Mzee Gamba na mkewe pamoja na mtoto wao wakawa wametulia tuli wakiangalia
“Anaitwa Ashura vilee enhee..?” Ostaadh aliuliza bila kuinua kichwa kutaka uhakika wa jina. Baada ya kuitikiwa kwamba ni sahihi akaendelea kusoma kile kitabu kwa lugha ya kiarabu. Baada ya dakika kadhaa akainua uso akamwambia Ashura ampe mkono wa kulia. Ashura akafanya hivyo, hapo Ostaadhi hakuendelea kuangalia kile kitabu, badala yake akamkazia macho Ashura huku amemshika mkono na kuendelea kuongea maneno kwa lugha ile ile. Baada ya hapo akamuachia mkono na kumshika kichwa huku akiendelea kuongea maneno ya kiarabu aliyokuwa akiyajuwa yeye mwenyewe. Ghafla machozi yakaanza kumtiririka Ashura kama mtu aliyefungua koki ya bomba la maji, hakua akilia kwa sauti..bali ni machozi tu yaliyokuwa yakimwagika yenyewe. Baaada ya dakika kama tano Ostaadh akaondoa mkono kichwani mwa Ashura na kunyamaza kama sekunde tatu kisha akashusha pumzi nzito kama tairi la gari linalopata pancha ghafla! Akajiweka vizuri kisha akasema
“Mtoto wenu ana tatizo kubwa..” Alinyamaza kidogo kisha akaendelea “Na kusema ukweli mimi binafsi sina uwezo wa kulimudu tatizo hili!..kwanza najisikia kuogopa kwa hili nililoliona hapa”
“Ostaadh sijakuelewa..una maana gani?!” Alihoji kwa mshangao Mama Ashura kama mtu asiyetaka kukubaliana na kile anachokisikia. ( Kutoka Msanga kwenda Kimanzichana ni mwendo wa saa moja na nusu kwa pikipiki, kwa miguu inaweza kuchukua mpaka masaa sita.)
“Bwana Jengo ebu tuweke wazi..nini tatizo?!” Aliongeza Mzee Gamba
“kama nilivyosema mwanzo kwamba, tatizo la mwanenu ni kubwa na mimi uwezo wangu wa kulimaliza tatizo hilo ni mdogo mno..” Alijibu Ostaadh Jengo na kuendelea “Nitakachowasaidia nitampa dawa ya kutuliza tu kwa leo..baada ya hapo naona mngefunga safari ya kwenda kimanzichana, kule kuna wataalamu wakubwa zaidi yangu ambao labda wanaweza kuwasaidia zaidi!” Alimaliza kuongea huku akinyanyuka akiwaacha wazazi wa Ashura midomo wazi kwa kutofahamu nini kinaendelea, akafunua kinu kilichokuwa pembeni akatoa majani, akamkabidhi mama Ashura
“Hii dawa mkifika nyumbani mchanganyie na maji ya moto kisha muogeshe na nguo zake hizi hizi..sawa?, halafu maji mengine utamuwekea kwenye kiganja chake atakunywa mara tatu. Dua nililomfanyia hapa pamoja na hii dawa vitamsaidia kumtoa joto na atatulia kabisa, lakini kesho mfanye mpango mumpeleke Kimanzichana kule kuna wakubwa zangu watamsaidia kumaliza tatizo!” Alisema Ostaadh Jengo kwa kumaanisha kile alichokuwa akikiongea
ITAENDELEA>>
NI TATIZO LIPI KUBWA LILILOMKUMBA MTOTO ASHURA MPAKA OSTAADH KUFIKIA KUOGOPA NA KUSHINDWA KUMTIBU? WATAWEZA KWENDA KIMANZICHANA? ITAKUWAJE..? Usikose sehemu ya tatu ya muendelezo wa Simulizi hii ya kusisimua keshokutwa Jumapili saa 12 jioni
SIMULIZI: JOHNSON NA MARIA
Posted by: Unknown Posted date: 9:30 PM / comment : 0 SIMULIZI
SIMULIZI: JOHNSON NA MARIA
Posted by: Unknown Posted date: 9:20 PM / comment : 0 SIMULIZI
SIMULIZI: JINI CHEKETU SEHEMU YA PILI Na Amir Malick
Posted by: Unknown Posted date: 6:19 PM / comment : 0 SIMULIZI

ILIPOISHIA:
Macho yalikuwa yamebadirika rangi na kuwa myekunduuu kama amemwagiwa maji ya pilipili kiswasa! Mishipa ya kichwa ilikuwa imemsimama kisawasawa na pua zikawa zinamcheza kama nguruwe pori anayegombana na shina la muhogo. Alikaza macho na kumuangalia mama yake kwa sekunde kumi, alipohakikisha kuwa ni mama yake kweli, tena mama yake mzazi.. huku machozi yakimtoka akajitahidi kujaribu kufungua midomo na kuanza kusimulia kilichomkuta.
ENDELEA
Ashura alianza darasa la kwanza akiwa ni mwenye bidii nyingi mno, hakukatishwa tamaa na umri wa miaka kumi aliokuwa nao, wala hakuchoshwa na hali ya baridi la alfajiri na kulowa umande kwenda shule, mwendo wa kilometa mbili aliokuwa akitembea kila siku alikuwa ameshauzoea. Alisoma kwa bidii na kujituma zaidi kwenye masomo na ndani ya kipindi kifupi tu kila mtu kijijini hapo alipata habari zake juu ya ufanisi wake mzuri darasani, wazazi wake walifurahi na kuamini wamepata mkombozi wa maisha yao baada ya kaka zake wote kutimkia mjini karibu miaka mitano iliyopita huku wakiwa hawana elimu, wala maisha yoyote mazuri zaidi ya kutangatanga na jiji bila ya kuleta chochote kijijini kwa wazazi wao.
“Soma mwanangu..wewe ndo tunakutegemea uje kutuokoa wazazi wako hapo baadae” alisema mama Ashura akimwambia mwanawe huku akipekuwa daftari la hesabu na kuona amekosa hesabu moja tu kati ya hesabu kumi walizofanya siku hiyo
“Kama hujaelewa uwe unamuuliza mwalimu atakuelewesha..sawa? na usiwe mgomvi kwa watoto wa watu wala usijiingize kwenye makundi ya wanaume! Sawa mwanangu?..wanaume wana ‘ukimwi’ watakuambukiza utakufa!!” Mara kwa mara alikuwa akitumia muda mwingi kumsihi mwanawe na hata inapobidi kutumia vitisho vikali ili kumuhepusha kujiingiza katika makundi yasiyofaa na kuharibikiwa
Ilikuwa imeshatimu saa saba kamili mchana ambapo wanafunzi wote wanaruhusiwa kurudi majumbani mwao.
Kama ilivyo kawaida Ashura na baadhi ya marafiki zake wakajikusanya, walipo hakikisha wametimia, wakaanza safari ya kurudi nyumbani. Mwendo wa kama dakika kumi na tano Ashura akajikuta amebaki peke yake baada ya marafiki zake wote kila mmoja kuchapuka njia yake kuelekea kwao. Mara zote alijisikia mnyonge kutengana na rafiki zake hao, alitamani wangekuwa wanarudi wote mpaka nyumbani na kuishi pamoja kila siku, kwani alishawazoea kucheza michezo ya hapa na pale njiani..wakati mwengine alijipa moyo kwamba kesho watakutana tena, akawa kila wanapoachana anaombea asubuhi nyingine ifike ili aweze kwenda shule na kuonana nao. hiyo nayo ikawa ni sababu nyengine kubwa iliyomfanya azidi kuipenda shule. Hivyo hakuwa na jinsi kwani kila mtu alikuwa ameshafika kwao na kubaki yeye peke yake kuendelea na safari kurudi nyumbani. Mkononi akiwa ameshika mfuko wa naironi wenye rangi ya bluu( maarufu kama mfuko wa rambo ) ambao alikuwa amebebea madaftari yake ya shule
Safari aliyokuwa amebaki nayo ilikuwa ndefu kidogo, hivyo hakutaka tena kuendelea na michezo ya njiani ukizingatia alikuwa yuko peke yake, alinyoosha moja kwa moja akiifuata njia nyembamba iliyokatiza katikati ya pori kuelekea nyumbani. Njaa ilikuwa ni sababu nyengine iliyomfanya azidishe mwendo kuwahi chakula. Jua kali la saa saba mchana lilikuwa linawaka na kufanya barabara kukakamaa na kuwa ya moto! Tangu ahaidiwe kuwa ataletewa viatu vya shule na shangazi yake anayeishi Majoye jijini Dar es Salaam ni muda mrefu umepita bila kuletewa hata kandambili moja, hivyo akawa hana jinsi kwenda shule pekupeku, jua likazichoma nyao zake kisawasawa!
“Shikamoo bibi” Alimwamkia bibi mmoja aliyekutana naye njiani huku akisimama na kusogea pembeni kumpisha bibi yule apite kwanza kisha na yeye ndio apite. Hiyo ni moja ya tabia na heshima ambazo karibu watoto wote wa vijijini wanafundishwa kuifuata
“Marahabaa mjukuu wangu..ndio unatoka shule?” Bibi aliitikia salamu ile na kumuuliza huku akiwa amekunyata mikono yake nyuma. Alikuwa ni bibi mzee sana mwenye umri wa miaka inayofikia themanini na zaidi. Uzee aliokuwa nao ulimfanya apinde mgongo na kumfanya kuwa na kimo kifupi huku akitembea kwa hatua fupi na mwendo wa taratibu mno. Ashura hakuwa anamjua bibi huyu, ila alimsalimu kwa heshima kama bibi yake
“Ndio bibi natoka shule narudi nyumbani” Alijibu Ashura. Baada ya hapo kimya kikatanda.
Ni tofauti na alivyokuwa akifikiria Ashura labda yule bibi angeongeza sentesi nyengine au kumuuliza ama kumwambia kitu kingine chochote baada ya kumjibu lile la kwanza..lakini yule bibi hakuuliza tena swali lingine na wala hakuonyesha kama alikuwa anaongea na Ashura, badala yake akampita taratibu na kuendelea na safari yake kimya kimya. Japo alikuwa ni mtoto mdogo lakini aliweza kushangazwa na hilo ambalo kwake aliliona si la kawaida, baada ya kumpita hatua kama tatu akajikuta anageuka nyuma na kumuangalia vizuri yule bibi, lakini ajabu hata alipogeuka hakumuona! Aliangalia ile njia yote ilikuwa nyeupee lakini yule bibi haonekani! Ashura alishangaa maajabu yale. Akavuta kumbukumbu zake haraka haraka akaamini kwamba alikuwa anaongea na bibi sekunde nne tu zilizopita, na yule bibi alikuwa anaelekea kule ambapo yeye alikuwa anatoka..sasa iweje wapishane sekunde hii hii na sekunde hii hii asimuone tena!? Ukizingatia mwendo aliokuwa akitembee yule bibi ni mwendo wa kujikongoja mno ambao hata sisimizi angemvuka! Kweli uzee aliokuwa nao angeweza kutembea haraka kwa speed ipi mpaka kumaliza njia yote bila kuonekana!? Tena ni njia ambayo imenyooka ya kuweza kumuona mtu hata aliyekuwa umbali wa mita mia mbili! Inakuwaje yule bibi asionekane?!
“Ina maana ameyayuka?!” Aliwaza lakini hakutaka kuamini hilo moja kwa moja. Alijaribu kuangalia tena huku na huko labda pengine atakuwa amechapuka njia nyingine..lakini hakukuwa na njia nyingine zaidi ya hiyo. Alitamani kumuita lakini akasita. Alitulia akabana pumzi kama sekunde tatu akisikilizia kwa umakini mkubwa kama atasikia hata ishara yoyote ya yule bibi akitembea..lakini wapi! Eneo lote lilikuwa kimya na hakukuwa na mtu mwingine yoyote zaidi ya yeye Ashura peke yake. Akahisi mwili unamwisha nguvu na mapigo ya moyo yakaanza kwenda kasi kwa uoga
****************** ********************* *********************
“Yule bibi ndio sijamuona tena!.. na mimi hapo hapo kichwa ndio kikaanza kuniuma ndio nikakimbia..” Kwa kukwama kwama Ashura akamaliza kumuadithia mama yake kile kilichomtokea njiani huku machozi yakimtoka. Mama yake akashusha pumzi nzito akajuwa mwanawe amepatwa na tatizo.
“Loh! Pole mwanangu.. lakini sasa hivi unajisikiaje?”
“Kichwa kinazidi kuniuma mamaa..”Alisema Ashura huku akilia “Mwili hauna nguvu na miguu mizitoo..halafu naona kizunguzungu”
Mh! Mama yeke akastuka, akafikiria haraka haraka akaona anatakiwa atoe msaada kwa mtoto wake haraka sana la sivyo mambo yanaweza kubadilika muda si mrefu. Kwani joto lilizidi kuongezeka na Ashura kuzidi kuregea. Akafikiria dawa ya kumpa lakini akakumbuka ndani hakukuwa hata na nusu ya kidonge cha panado. Akapata jibu ni lazima ampeleke kwa mtaalamu wa jadi haraka sana! Akatoka nje kuangalia kama anaweza kupata msaada hata wa mpita njia mwenye baiskeli ili aweze kumsaidia kumbeba..lakini hakuna mtu aliyekuwa anapita barabarani! Akawa kama amechanganyikiwa, hajui nini afanye kumuokoa mwanae, kila nyumba ya jirani aliyofikiria kwenda ilikuwa mbali na akili haikumruhusu kwenda mbali huku akimuacha mwanawe peke yake katika hali ile. Kengere ikagonga kichwani mwake kwamba mwanawe yupo kwenye hali tete!
“Huyu baba yako naye tabia zake hizi sijui ataziacha lini?!” Alisema peke yake kwa hasira mama Ashura huku akijaribu kuchungulia huku na kule kama atapata hata msaada wa mpita njia pale nje
“Ye kila akienda shambani muda wa kurudi hafiki nyumbani kwake kwanza mpaka apitie vijiweni..matokeo yake ndio kama hivi mi nipo peke yangu hapa sasa nafanyaje eeng’?!” Alizidi kuhamaki na kupagawa huku akimtupia lawama mume wake ambaye mpaka muda huo alikuwa bado hajarudi kutoka shamba
“MAMAA.. MAMAAAAAAAAAAAAA….!!!” Kelele zilisikika kutoka ndani alipokuwa Ashura. Mama yake akakurupuka mbio kurudi ndani kujuwa nini kilichomfanya mwanawe kupiga kelele zile
“Vipi?..kuna nini!?..Ashura! Ashuraa!! We Ashura!!!” Aliuliza kwa mshangao na kuita huku akiwa amemshika mabegani na kumtingisha. Lakini masikini Ashura wala hakuonekana kutingishika wala kupepesa macho, badala yake akawa ameganda amebutua macho tu kama mtu aliyekuwa akiona maajabu ya mwisho ya Dunia.
“Ashuraaa!!!” Aliita tena bila mafanikio
ITAENDELEA IJUMAA SAA 12 JIONI
JE ASHURA AMEPATWA NA NINI? MZIMA AU AMEKUFA? MAMA YAKE ATAFANYAJE?
USIKOSE SEHEMU YA TATU YA SIMULIZI HII YA KUSISIMUA
SIMULIZI: JOHNSON NA MARIA
Posted by: Unknown Posted date: 9:24 PM / comment : 0 SIMULIZI
Maria alitoa mfuko uliokuwa na chips kuku akampa Johnson akamuambia asihangaike kupika. Johnson alifurahi sana akamtania Maria akamwambia "sijui kama siku nikiwa jela utaniletea vitu kama hivyo"
SIMULIZI: JOHNSON NA MARIA
Posted by: Unknown Posted date: 10:04 PM / comment : 0 SIMULIZI
SIMULIZI: JINI CHEKETU SEHEMU YA KWANZA
Posted by: Unknown Posted date: 7:18 PM / comment : 0 SIMULIZI

Simulizi kali ya kutisha iliyoandikwa na Amir Malick, imeanza leo sehemu ya kwanza. Fuatilia na usikubali kupitwa na simulizi hii ya kusisimua hapa hapa kwenye ukurasa huu
STORY: JINI CHEKETU
MTUNZI: AMIR MALICK
MOBILE: 0719-050588
Ghafla kichwa kikaanza kumuuma. Jasho likaanza kumtoka na miguu kuishiwa nguvu kama mtu aliyepigwa na marungu mazito!, alitamani kukaa chini lakini maumivu makali ya kichwa yaliyokuwa yakizidi kila baada ya sekunde yalimfanya atupe chini mfuko wake wa rambo ambao alikuwa amebeba madaftari yake ya shule na kushika kichwa..alitaka kupiga kelele lakini alihisi koo limemkauka na hakuna ukelele wowote ambao angeweza kuutoa! Mwili ukamuisha nguvu na mapigo ya moyo kumuenda kasi..aliogopa sana lakini hakujuwa anachokiogopa. Aligeuka kushoto na kulia kama mtu anayetafuta njia ya kutokea..lakini hakuiona, alihisi kama anaguswa mgongoni..aligeuza mwili mzima mzima na kugeuka nyuma kwa kasi..lakini hakuona mtu. Woga ulizidi kumjaa, mwili ukazidi kumtetemeka. Hakuona msaada wowote zaidi ya pori kubwa lililomzunguuka na kuacha kinjia kidogo chembamba kilichonyooka. Jua la saa saba lilizidi kumchoma na kuhisi kama kichwa kinataka kupasuka, vivuli na mivumo ya miti vilizidi kumchanganya, sauti za ndege waliokuwa wakilia kwenye pori lile zilionekana kuzidi kumtisha. ASHURA hakuwa kabisa kwenye Dunia hii tuliyopo sisi..bali alikuwa kwenye dunia nyengine ya ajabu ambayo hata hakuweza kutambua aliingiaje. Umri wake mdogo wa miaka kumi lakini aliweza kutambuwa kwamba yupo kwenye hatari kubwa. Hatari ambayo inaisakama maisha yake. Masikini ya Mungu hakuweza kujuwa afanyaje katikati ya pori lile. Akapata wazo moja tu.. “KUKIMBIA”
Akarudia tena kuangalia mazingira yaliyokuwa yamemzunguuka koshoto na kulia, bila ya kukumbuka mfuko wake wenye madaftari ya shule ambao ameubwaga pale chini.. kama mtu aliyechanganyikiwa akatimua mbio kwa kasi ya ajabu kuifuata njia ile nyembamba. Njia ambayo anaipita kila siku tangu siku ya kwanza anaanza darasa la kwanza katika shule ya Msingi Msanga Mtimle..tena akipita kwa madaha yote! lakini leo ajabu imekuwa tofauti na kujikuta yupo katika hali asiyoielewa
Tangu alipoanza mbio zile hakufikiria kuangalia pembeni wala kugeuka nyuma, badala yake alichokuwa akikihitaji ni kufika nyumbani tu. Hakuweza kukutana na mtu yoyote njiani..hakufikiria kusimama popote pale, kwani aliamini hana njia nyengine ya kujiokoa zaidi ya kukimbia, hata alipojaribu kujiuliza sababu iliyokuwa ikimfanya akimbie hakupata jibu sahihi..lakini nafsi yake ilimuamuru hivyo..na hakuona sababu ya kupinga, alizidi kuongeza kasi huku akiwa ametawaliwa na woga mkubwa.. ilimchukuwa kama dakika kumi akawa amefika nyumbani kwao. Hakutaka hata kusimama pale kwenye uwanja wa nyumbani kwao, badala yake kwa kasi ya kimbunga akampita mama yake mzazi aliyekuwa amekaa kwa pembeni akiosha vyombo.. akapitiliza moja kwa moja mpaka ndani kwenye kijumba chao cha udongo. Na kama laiti ile nyumba ingekuwa ina mlango mwingine wa kutokea uani,,basi angepita na kuendelea kukimbia
“We Ashuraa!!!” aliita mama yake kwa taharuki huku akiwa hana uhakika kama aliyepita pale kwa kasi ile ni Ashura kweli ama lah..!
“Ashuraaaa..!” Aliita tena bila kujibiwa. Alipoona hajibiwi ikabidi anyanyuke, akaangalia kule alipotokea Ashura kama pengine palikuwa na mtu anamkimbiza au kitu chochote kilichomfanya mwanawe akimbie vile, lakini hakuona kitu, akakaguwa tena huku na huko lakini wapi hakukuwa na kitu.
“Tayari hivyo ushachokoza watoto wa watu unakimbilia ndani..!!” Alisema mama Ashura kama kujaribu kuhisi labda jibu lingekuwa sahihi na alivyofikiria kwamba Ashura anakimbia baada ya kuanzisha ugomvi na watoto wenzie huko alipotoka. Ni kawaida kwa watoto kucheza na kugombana hiki na kile na hata kufikia kukimbizana. Huku akijifunga khanga yake vizuri mama Ashura akuvuta hatua za haraka haraka kuelekea ndani
Kama mtu anayeanzwa na uchizi wa ghafla, alijikusanya akajibana kwenye pembe ya ukuta wa udongo mwisho kabisa kwenye chumba kile bila kujali kama anachafua shati lake jeupe la shule alilolivaa, huku vipande vya udongo na vumbi vikiwa vinamdondokea.. akavuta shuka kubwa kuukuu ambalo lilikuwa halieleweki hata rangi yake baada ya kuwa la zamani mno na hata kuchakaa toka pale kwenye kitanda chao kidogo cha kamba, akajikunja kama paka aliyenyeshewa na mvua, akajifunika gubigubi akatulia kimya
“Ashura!” Aliita tena mama yake baada ya kuingia ndani na kumuona mwanawe akiwa amejificha kule pembeni bila ya kuonekana hata unywele mmoja. Taratibu kwa tahadhari yenye uwoga akasogea mpaka pale alipokaa Ashura, akafunua lile shuka kwa kutumia nguvu kidogo. Akamkuta Ashura anatweta huku akitetemeka mwili mzima, hakuonekana kutoka jasho japo alitoka kukimbia mbio ndefu. Akawa ameendelea kujikunja vile vile huku kichwa chake akiwa amekifutika kwenye magoti yake na kujizunguushia mikono yote miwili. Hali ile ilizidi kumchanganya mama yake asijuwe mwanawe amepatwa na nini, hakuna hata siku moja aliyowahi kurudi akiwa katika hali hii, leo imekuwaje tena! Akatoka nje tena akaangalia mazingira kama kuna chochote kinachokuja upande wa nyumba yao..lakini hakuona kitu. Alipohakikisha kwamba kupo sawa akaingia tena ndani kisha akasindika kimlango chao kilichokuwa kimefumwa kwa makuti, na kwenda tena pale alipo mwanawe
“We Ashura..mbona hivyo! Kulikoni?” Ashura hakujibu kitu wala kutikisika badala yake alitulia tuli vile vile
“Ashura mwanangu mi naongea na wewe..ebu niambie kuna nini?!” Alihoji tena mama yake kwa shauku kubwa ya kutaka kujuwa sababu ya mwanawe kuwa katika hali ile. Alipoona hajibiwi akamshika kichwa na kujaribu kumuinua uso wake. Kichwa cha Ashura kilikuwa cha moto kama chungu kilichotoka kuepuliwa jikoni, mama yake akagundua hilo. Akahisi mwanawe yupo kwenye tatizo, akakaa chini
“Ashura mwanangu..mimi ni mama yako ebu niambie una nini?!” Alishusha sauti huku akimsogeza mwanawe na kumkumbatia kujaribu kumtoa hali aliyokuwa nayo ili aweze kumwambia kilichomsibu. “walitaka kukubaka..?” Muda wote huo Ashura alikuwa amenyamaza kimya huku akitetemeka na joto kuzidi kuutawala mwili wake. Alionekana ni mwenye hofu kubwa sana na kuna vitu vilikuwa vinapita kichwani mwake kama mkanda wa sinema..lakini kila akitafakari kupata jibu ya vitu vile hakuweza kuambua kitu, tena kila alipozidi kufikiria aliona kiza kizito kinatanda mbele na kufanya macho yake kupoteza nuru taratibu. Alikuwa anatamani kumwambia mama yake lakini alihisi mdomo usingefunguka..au hata kama ungefunguka basi sauti isingetoka.. na kama sauti ingetoka basi maneno yasingeeleweka. Alijaribu kuanza kupangilia maneno lakini alihisi mdomo umeshonwa nyuzi nyingi nzito zinazofanya ashindwe kuinua midomo!.. mara aliona kama kuna mtu amemsimamia anamkataza asiseme kitu. Akajikakamua akameza funda la mate, akageuza shingo akamuangalia mama yake usoni kwa macho makali yenye mshangao kama vile anataka kuhakikisha kwamba yule aliyopo pale ni mama yake kweli ama lah..,macho yalikuwa yamebadirika rangi na kuwa myekunduuu kama amemwagiwa maji ya pilipili kiswasa! Mishipa ya kichwa ilikuwa imemsimama kisawasawa na pua zikawa zinamcheza kama nguruwe pori anayegombana na shina la muhogo. Alikaza macho na kumuangalia mama yake kwa sekunde kadhaa, alipohakikisha kuwa ni mama yake kweli, tena mama yake mzazi.. huku machozi yakimtoka akajitahidi kujaribu kufungua midomo na kuanza kusimulia kilichomkuta.
JE ASHURA AMEKUTWA NA NINI? ATAWEZA KUSEMA NA KUMWAMBIA MAMA YAKE? FUATILIA TENA SEHEMU YA PILI YA SIMULIZI HII SIKU YA KESHO KUTWA JUMANNE
JOHNSON NA MARIA
Posted by: Unknown Posted date: 9:34 PM / comment : 0 SIMULIZI
Johnson aliwahi asubuhi kama kawaida yake akaanza kujiandaa kwa ajili ya kwenda gengeni kwake akamwambia Maria awahi kwenda kwao kabla wazazi wake hawajarudi
JOHNSON NA MARIA
Posted by: Unknown Posted date: 9:38 PM / comment : 0 SIMULIZI
Ilipoishia
Johnson aliwahi asubuhi kama kawaida yake akaanza kujiandaa kwa ajili ya kwenda gengeni kwake akamwambia Maria awahi kwenda kwao kabla wazazi wake hawajarudi
JOHNSON NA MARIA
Posted by: Unknown Posted date: 9:33 PM / comment : 0 SIMULIZI
Ilipoishia
Johnson alirudi kazini saa 4 usiku akakuta anapowekaga funguo yake haipo alijiuliza maswali mengi sana aliposukuma mlango wake akakuta umefungwa kwa ndani akazidi kuchanganyikiwa alianza kugonga kwa hasira akasikia sauti ya Maria ndani inamkaribisha
JOHNSON NA MARIA
Posted by: Unknown Posted date: 9:16 PM / comment : 0 SIMULIZI
Ilipoishia
Johnson alimpiga marufuku Maria kukanyaga pale Gengeni kwake Maria akawa analia hakukubaliana na lile swala Hadi mzee Joseph jirani wa Johnon pale Gengeni alivyoona kama hamna maelewano kati ya Johnson na Maria akaenda kuwauliza kinachoendelea alivyoelezewa akaanza kumpa somo Johnson
JOHNSON NA MARIA
Posted by: Unknown Posted date: 9:10 PM / comment : 0 SIMULIZI
Ilipoishia
Wazazi wa Maria walimuachia Johnson hakuamini macho yake hakutaka tena kwenda gengeni kwake alienda kwake kupumzika huku anawaza kutojihusisha kimapenzi na Maria tena wakati anawaza hivyo simu yake ikaita kucheki alikuwa ni Maria
JOHNSON NA MARIA.............COX DAWA YAO ORIGINAL
Posted by: Unknown Posted date: 10:08 PM / comment : 0 SIMULIZI
Ilipoishia
Wazazi wa Maria walitaka kumpeleka Johnson Kituo cha polisi lkn housegirl wao akawapigia simu akawaambia Maria kasharudi nyumbani walifurahi sana wakajadiliana waende na Johnson hadi nyumbani kwao ili wakajue kinachoendelea kati yake yeye na Maria
JOHNSON NA MARIA........COX DAWA YAO ORIGINAL
Posted by: Unknown Posted date: 10:00 PM / comment : 0 SIMULIZI

Baba yake Maria alimtolea Johnson bastola akamuambia "kijana usiposema binti yangu alipo leo nakumaliza " Johnson alibaki anatetemeka hajui afanye nini tangu azaliwe Akuwahi kuiona bastola akawa anafikiria kuwaambia wazazi wa Maria ukweli ili wamuachie
JOHNSON NA MARIA.........COX DAWA YAO ORIGINAL
Posted by: Unknown Posted date: 9:20 PM / comment : 0 SIMULIZI

Ilipoishia
Wazazi wa Maria walizidi kumtukana sana Johnson ndani ya gari Baba yake Maria akamuambia Johnson "Yani kijana tukimkuta binti yetu huku kwako leo ndo utakuwa mwisho wa maisha yako hatuwezi kukubali kijana masikini kama wewe huna mbele wala nyuma uwe mpenzi wa binti yetu''
- Popular Post
- Video
- Category
PelĂculas populares
-
Simulizi kali ya kutisha iliyoandikwa na Amir Malick, imeanza leo sehemu ya kwanza...
-
ILIPOISHIA: “MAMAA.. MAMAAAAAAAAAAAAA….!!!” Kelele zilisikika kutoka ndani ali...
-
ILIPOISHIA: Macho yalikuwa yamebadirika rangi na kuwa myekunduuu kama amemwagiwa maji ya p...
-
MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA III – (NAFASI 100) Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
-
Ilipoishia Maria alimpigia Johnson simu akamwambia anataka akalale tena nyumbani kwake Johnson akamgomea akamwambia asije sababu waz...
-
COMPUTER SYSTEM ANALYST II (MOBILE APPLICATIONS DEVELOPMENT/PROGRAMMER) POSITION DESCRIPTION: COMPUTER SYSTEM ANALYST II (...
-
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte) limesema kuanzia mwaka huu wa masomo, wanafunzi wanaotaka kujiunga na masomo ngazi ya astasha...
-
Ilipoishia Wazazi wa Maria walitaka kumpeleka Johnson Kituo cha polisi lkn housegirl wao akawapigia simu akawaambia Maria kasharudi nyu...
-
Ilipoishia Mzee Joseph akamuambia Maria "Binti umependeza sana we mrembo kweli Johnson anajua kuchagua" Maria akacheka kusikia...
-
The Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) is focusing on increasing the outreach and service quality of its Energy products f...













