ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5

KLABU YA DARAJA LA KWANZA YAMSAJILI RAIS WA BOLIVIA KATIKA NAFASI YA KIUNGO


Timu moja ya soka ya wachezaji wa kulipwa ya nchini Bolivia imemsajili rais Evo Morales kama mchezaji wao kiungo atakayeichezea timu hiyo katika msimu ujao.

Morales mwenye miaka 54 ni shabiki mkubwa wa soka, na msimu ujao ataichezea klabu ya Sport Boys, yenye maskani yake kusini-mashariki mwa mkoa wa Santa Cruz.

Timu hiyo ya daraja la kwanza imesema rais Morales atakuwa anacheza soka kwa dakika 20 tu katika mechi moja lakini si kila mchezo kutokana na ratiba yake ya majukumu ya taifa.

Rais Morales atakuwa atalipwa na kabu hiyo mshahara wa kiasi cha dola 214.

ARSENAL YATOA JEZI KUSHEREHEKEA MIAKA 20 YA UHUSIANO NA NIKE

KLABU ya Arsenal imetoa jezi mpya baada ya kutwaa Kombe la FA kusherehekea miaka 20 ya uhusiano wao na Nike ambao umefikia tamati mwishoni mwa msimu huu. Ni jezi yenye mwonekano tofauti na jezi za miaka mingi iliyopita Arsenal na zinakuja baada ya kumaliza ukame wa miaka tisa wa mataji.
The Gunners walitwaa Kombe la FA Jumamosi baada ya kuifunga Hull City 3-2 ndania ya dakika 120 Uwanja wa Wembley.

NEMANJA VIDIC APEWA MKONO WA KWAHERI MAN UNITED OLD TRAFFORD

Beki  na nahodha wa Manchester United, Nemanja Vidic ameagwa rasmi leo Old Trafford baada ya kuitumikia klabu hiyo katika mchezo wa mwisho wa nyumbani msimu huu na kushinda mabao 3-1 dhidi ya Hull City.
Vidic amepewa zawadi ya shukurani kwa utumishi wake wa miaka nane katika klabu hiyo, huku akiwa tayari alishaaga.
Beki huyo alipewa zawadi hiyo na Sir Bobby Charlton kabla ya vijana wa Ryan Giggs hawajaanza mechi.
Hata kama beki huyo mwenye miaka 32 alianzia benchi katika mechi ya leo, lakini alipata nafasi ya kucheza kwa mara ya mwisho Old Trafford.
All smiles: Nemanja Vidic was given a present by Sir Bobby Charlton at Old Trafford on Tuesday night

WAJUMBE TFF WAKATAA TIMU 16

Dar es Salaam. Jaribio la kuzipandisha klabu za Mwadui na African Lyon kinyemela limegonga mwamba baada ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kugoma kuongeza timu za Ligi Kuu hadi 16 msimu ujao wa 2014/2015.
TFF ilitaka kuongeza timu hadi kufikia 16 kwa lengo la kuipoza Mwadui ambayo ilipokwa nafasi ya kucheza Ligi Kuu baada ya Stand United kupewa pointi za mezani siku ya mwisho ya Ligi Daraja la Kwanza, wakati uongozi wa African Lyon unahusishwa kuwa na uhusiano wa karibu na ‘bosi’ mmoja wa TFF.

DIOP ALICHOWAFANYIA MASHABIKI WA ATLETICO MADRID

Ubaguzi wa rangi umezidi Hispania, baada ya mchezaji wa Levante, Pape Diop kuzomewa na kufanyiwa ishara za nyani jana na mashabiki wa Atletico Madrid wakati wa mechi ya La Liga.
Wiki moja baada ya beki wa Barcelona, Dani Alves alipolazimika kula ndizi aliyotupiwa na mashabiki, kiungo huyo wa Senegal alisema alicheza kama nyani mbele ya waliomzomea na kumkebehi.
"Waliniita nyani,niligeukia na kujifanya nyani," alisema Diop na kukaririwa na Marca.com. "Nimechoka na ubaguzi katika soka. Na upo mwingi.
 Wachezaji wa Atletico, Diego Godin na Diego Costa wakimfuata Diop anayeshangilia kwa kucheza kama nyani

RONALDO AINUSURU REAL MADRID DAKIKA ZA MWISHONI

Cristiano Ronaldo jana alifunga bao tamu sana na kuinusuru Real Madrid kupoteza mechi.
Valencia ilionekana kubeba pointi zote tatu Uwanja wa Santiago Bernabeu, lakini mshindi huyo wa Ballon d'Or aliinusuru timu yake tena, alipounganisha krosi ya Angel di Maria kwa utaalamu wa hali ya juu. 
Mathieu alianza kuifungia Valencia dakika ya 44, lakini Sergio Ramos akaisawazishia Real Madrid dakika ya 59na Parejo akawafungia wageni bao la pili, kabla ya Ronaldo kufunga lake la 50 msimu huu. 
Licha ya Atletico kufungwa 2-0 na Levante jana, bado ipo kileleni mwa La Liga kwa pointi zake 88 za mechi 36, ikifuatiwa na Barcelona pointi 85 mechi 36 wakati Real sasa ni ya tatu kwa pointi zake 83 za mechi 35. 
 Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefunga bonge la bao jana katika sare ya 2-2 na Valencia

BAADA YA KAVUMBAGU NA DOMOYO KUTIMKIA AZAM, MOSHA AFUNGUKA

10302029_722357961140073_1520041417937471076_n

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MAKAMU mwenyekiti wa zamani wa Yanga sc, Bilionea, Davis Mosha ameushutumu uongozi wa sasa wa klabu hiyo kushindwa kuwabakiza wachezaji muhimu kikosini kuelekea msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara na michuano ya kimataifa.
Mosha ambaye ni mwanachama na shabiki mkubwa wa Yanga, ameshangazwa na uongozi wa klabu hiyo chini ya mwenyekiti Yusuf Manji kumwachia kiungo wake mkabaji, Frank Domayo na mshambuliaji Didier Kavumbagu  kwenda Azam fc.

WILAYA YA CHUNYA YAANZA KUJENGA UWANJA WA MICHEZO


Ramani ya uwanja wa mpira wa miguu na riadha

KAVUMBAGU ASAINI AZAM

                    
                             Kavumbangu akitia dole gomba Mkataba wa Azam leo
 
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
NAHODHA wa Burundi, Didier Kavumbangu amesaini Mkataba wa miaka miwili na mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC mchana wa leo, BIN ZUBEIRY imeipata hiyo.
Kavumbangu aliyemaliza Mkataba wake wa miaka miwili Yanga SC, ameamua kusaini Azam FC baada ya kuona klabu yake haina mawasiliano naye licha ya kumaliza Mkataba wake.
“Mimi ni mchezaji, kazi yangu ni mpira. Nimemaliza mkataba Yanga, lakini viongozi hawaniambii kitu, nimepata ofa nzuri Azam nikaamua kusaini,” amesema Kavumbangu akizungumza baada ya kusaini Mkataba huo ambao unamfanya alipwe vizuri kuliko alivyokuwa analipwa Jangwani.

ALIYEKUWA KOCHA WA BARCELONA AFARIKI DUNIA

RIP Tito Vilanova, who has died aged 45 -- http://bit.ly/1rtyw2s
The Barcelona coach has been battling with cancer for a few years now, but surgery on Thursday was unable to save his life.

AZAM KUVUNA 75M ZA UBINGWA KUTOKA VODACOM

Meneja uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa kutangaza zawadi za washindi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambapo Azam FC ambaye ndie bingwa atanyakua Milioni 75. Pamoja nae katika picha, wa kwanza kutoka kulia niAfisa Habari wa TFF, Boniface Wambura na Afisa Matukio na Udhamini wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude.

VIJANA 72 WAANZA MAFUNZO RASMI KUPITIA AIRTEL RISING STARS


 Kocha Andrew Stokes kutoka shule ya soka la vijana ya Manchester United, akitoa maelekezo kwa washiriki wa kliniki ya Kimataifa ya soka ya Airtel Rising Stars inayofanyika kwenye uwanja wa Azam Compex jijini Dar es Salaam.

BURUNDI KUWASILI KESHO KUMENYANA NA STARS

Timu ya Taifa ya Burundi (Intamba Mu Rugamba) inatarajiwa kuwasili nchini kesho (Aprili 24 mwaka huu) saa 12 jioni kwa ndege ya Kenya Airways tayari kwa mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumamosi (Aprili 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

WACHEZAJI WA AIRTEL RISING STARS KUTOKA SIERRA LEONE WAWASILI


 Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius mara ya kupokea timu ya Airtel Rising Stars kutoka Sierra Leone ambao watahudhuria kliniki ya soka ya kimataifa ya Manchester United itayoanza Jumatano, 23-27 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

REKODI ZA VIPIGO VYAMUONDOSHA MOYES MAN U, GIGGS AKABIDHIWA TIMU HADI MWISHO WA MSIMU

Mkufunzi mkuu na meneja wa klabu ya Manchester United David Moyes ametimuliwa.
David Moyes amefutwa kazi baada ya kushikilia usukuni wa klabu hiyo kwa miezi kumi tu.
Moyes, mwenye umri wa miaka 50, aliteuliwa na Ferguson kumrithi alipostaafu mwaka jana baada ya kuwa na klabu hiyo kwa miaka 26.Klabu hiyo hapo awali ilikuwa imekataa kuzungumzia udaku wa magezti kuwa Moyes atafutwa kazi kabla ya msimu kumalizika.
Writing on the wall: Moyes has seen United fail to qualify for the Champions League this season

DAVID MOYES KUTIMULIWA MANCHESTER UNITED


MATOKEO: EVERTON JEURI WAADABISHA MAN U

All over? Kevin Mirallas doubles Everton's advantage with a fierce effort into the bottom corner
All over? Kevin Mirallas doubles Everton's advantage with a fierce effort into the bottom corner

ARSENAL YAWAPIGA TATU HULL CITY NA KUJIKITA NAMBA NNE

Strike: Lukas Podolski celebrates scoring Arsenal's second goal of the game against Hull

Strike: Lukas Podolski celebrates scoring Arsenal's second goal of the game against Hull

MATOKEO: LIVERPOOL WAZIDI JISAFISHIA NJIA YA UBINGWA, SUAREZ BADO GOLI MOJA AINGIE KATIKA HISTORIA

So close now: Raheem Sterling scored twice at Carrow Road to put Liverpool within touching distance of a first League title in 24 years
So close now: Raheem Sterling scored twice at Carrow Road to put Liverpool within touching distance of a first League title in 24 years
⬆
Top