ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5


Ilipoishia
Wazazi wa Maria walimuachia Johnson hakuamini macho yake hakutaka tena kwenda gengeni kwake alienda kwake kupumzika huku anawaza kutojihusisha kimapenzi na Maria tena wakati anawaza hivyo simu yake ikaita kucheki alikuwa ni Maria


Endelea
Johnson alipata xana hasira kuona Maria ndo anampigia simu wakati amemsababishia matatizo ile siku nzima hajafanya kazi wala hajakaa kwa amani, hakutaka kuipokea ile simu aliikaushia lakini Maria hakukata tamaa alizidi tu kumpigia Johnson simu Johnson alitamani hadi aizime simu yake lakini akaona apokee asikie Maria anamuambia nini alivyopokea tu Maria akamuuliza "vipi mpenzi wangu mbona nakupigia simu muda wote huo hupokei" Johnson akamjibu "sikiliza nikuambie Maria mimi sio mpenzi wako tena na kuanzia leo sitaki tena unifuate fuate wazazi wako leo wamenipa sana tabu wameniaibisha wamenitukana na kunitamkia maneno ya dharau sana wewe tafuta tajiri mwenzako mimi niache sitaki kuyaweka maisha yangu hatarini kwa ajili yako"
Maria alivyosikia vile akaanza kulia kwenye simu "Johnson mimi na wewe tumetoka mbali sana mimi nakupenda kuliko mwanaume yoyote hapa duniani usiwasikilize wazazi wangu hawawezi kutuachanisha mimi na wewe na ukijaribu tu kuniacha mimi nakunywa sumu Johnson bora nife" Johnson kusikia Maria anaongea swala la kujiua akaona bora ampe moyo sababu akili ya Maria aliijua alikuwa akiongea kitu hatanii akajua Maria akinywa tu sumu kwa ajili yake akafa atapata msala mkubwa sana akamwambia "Maria najua unanipenda hata mimi nakupenda pia ila tatizo wazazi wako hawataki wewe uwe na mimi cha kufanya sasa hivi tutulie kwanza hadi wazazi wako wakijisahau ndo tuendelee na mapenzi yetu sababu wanapajua hadi ninapoishi unaweza siku ukaja huku ghafla wakatokea ikawa balaa"
Maria "baby najua unawaogopa sana wazazi wangu ila tambua kuwa mimi siwezi kuishi bila wewe hata wazazi wangu nimewaambia na wakiendelea kuyafuatikia mapenzi yetu mimi nitachukua maamuzi mabaya"
Yale maneno ya Maria yalimchanganya sana Johnson akampa moyo Maria hadi akatulia lakini bado yeye msimamo wake ulikuwa ni ule ule kuachana na Maria ili aishi mjini kwa amani
Ile siku nzima alishinda kitandani anafikiria kile kilichomtokea kesho yake asubuhi aliwahi gengeni kwake kama kawaida watu wote wa maeneo yale waliomuona wakati anasombwa na wazazi wa Maria walimfuata na kumpa pole huku wengine wakimshauri aachane na Maria asije akajitafutia matatizo. Mchana alishangaa kumuona Maria kamfuata tena pale gengeni kwake alikasirika sana akamuambia "we Maria mimi si nimekukataza kuja hapa baba yako na mama yako jana tu wamekuja kunisomba hapa gengeni kwangu kwa ajili yako leo tena umekuja hujui utanipa msala mimi"
Maria akamjibu "Sikiliza mpenzi wangu mimi nimeshakuzoea siku ikipita bila kukuona nahisi naumwa ndo maana kila nikitoka chuo lazima nipitie hapa gengeni kwako nikuone"Johnson mda wote huo anaongea na Maria macho yake yalikuwa yanaangaza pande zote alikuwa na wasiwasi wazazi wake Maria wanaweza kutokea. Johnson akamuuliza Maria "we Maria umefuata nini hapa gengeni kwangu wakati jana tu wazazi wako wamekuja kunisomba hapa kwa ajili yako " Maria akamjibu "Johnson hata wazazi wangu wafanye nini mimi siwezi kukuacha wewe na siwezi kupitisha siku bila kukuona huwa nahisi naumwa ndo maana nimekufuata hapa Gengeni"
Akili ya Johnson ilihama kabisa alihisi muda wowote wazazi wa Maria wanaweza kutokea pale au wakawa wameweka watu wawe wanawachunguza kama bado wanaendelea na mapenzi yao
Johnson akamwambia Maria "sikia Maria mimi bado akili yangu haijakaa vizuri kutokana na mambo yaliyotokea jana wazazi wako wameniaibisha sana wamenipotezea mda mwingi jana nimeshindwa hata kutafuta hela we nenda tutaongea siku nyingine na sitaki unifuate hapa gengeni kwangu ukiwa na shida na mimi nipigie simu tuongee"
Maria kusikia yale maneno akainamisha kichwa chini akaanza kutokwa na machozi akamuambia Johnson " Johnson we unajua kabisa mimi nakupenda sana mimi na wewe tumetoka mbali sana simjui mwanaume mwengine zaidi yako, unazani mimi nitawezaje kuachana na wewe kirahisi rahisi mimi ndio nimesema labda wazazi wangu waniue ndo tutaachana mimi na wewe" Johson na Maria walibishana sana pale mpaka wateja walikuwa wanakuja pale Gengeni na wapita njia wakawa wanawashangaa kumuona Maria analia ila watu wengi wa maeneo yale walikuwa wanajua Maria ni mpenzi wa Johnson sababu mara nyingi walikuwa wanawaona pamoja. Kuna mzee mmoja anaitwa mzee Joseph ana kiduka chake karibu na genge la Johnson alivyoona Johnson na Maria wanabishana sana akawafwata akawaambia "Samahanini vijana kwa kuingilia maongezi yenu mda mrefu sana naona kama mnalumbana hamuelewani hadi huyu dada muda wote analia kuna nini jamani? Johnson akaanza kumuelezea yule mzee mambo yote akamkumbushia hadi ile siku aliyokuja kufwatwa pale na gari akamuambia yule mzee "Mzee Joseph unakumbuka juzi kuna gari nyeusi ilikuja hapa kuna watu wakashuka wakanikamata wakaniambia nifunge genge wakaondoka na mimi wale ni wazazi wa huyu binti walitaka kunipeleka polisi bahati nzuri nikanusurika hawataki kabisa mimi niwe na mtoto wao sasa huyu mwenzangu mimi namuambia hanielewi ndo tunachobishana hapa. uYule mzee alimsikiliza Johnson kwa makini akamuambia "Nisikilize kijana ni kweli unavyofanya uko sahihi lakini mwenyewe unayajua mapenzi yalivyo mtu akikupenda anavyokua huyu binti anaonekana anakupenda kweli kutoka moyoni cha kufanya hapa ongea naye vizuri muelewane usikubali aondoke hapa na hasira anaweza akaenda kufanya kitu kibaya huko mwisho wa siku upate kesi kubwa zaidi ya hiyo"
Johnson alimsikiliza mzee Joseph kwa makini mda wote huo Maria alikuwa bado anamwaga machozi tu Johnson akamwambia yule mzee "Sikiliza mzee mimi sina uwezo hata wazazi wangu ni masikini sana wananitegemea mimi wazazi wake huyu binti ni maarufu sana hapa mjini ni watu wenye pesa mimi naogopa kufungwa nisije nikapotezwa bure"
Mzee Joseph akamuambia. Hata kama wazazi wake wana pesa mwenzio kashakupenda hvyo hvyo na umasikini wako kwenye mapenzi lazima kuwe na misukosuko ndo hiyo sasa unayoipata itabidi uvumilie ila tu muwe makini hao wazazi wake wasijue kama bado mnaendelea na mapenzi yenu"

Itaendelea


About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top