ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5



Ilipoishia Maria alipanda boda boda akaanza safari ya kwenda kwao Jonhson na yeye akapanda daladala akaanza safari ya kwenda gengeni kwake huku akimuomba mungu Maria awahi kufika kwao kabla wazazi wake hawajafika

Endelea Johnson alifika gengeni kwake akafungua akafanya usafi akaanza kupanga bidhaa zake. Alivyomaliza akatoa simu yake akampigia Maria ili ajue kinachoendelea huko nyumbani kwao Maria alivyopokea simu Johnson akamuuliza "vipi mpenzi wangu umefika salama nini kinaendelea huko?
Maria: "nashukuru Mungu nimefika salama mpenzi na nimewawahi baba na mama ila housegirl kaniambia jana usiku walimpigia simu wakamuuliza kama mimi nipo nyumbani akawajibu ndiyo nipo, Mama akamuambia anipe simu niongee naye housegirl akawadanganya nimelala nimekataa kufungua mlango wa chumbani kwangu" Johnson:  "Si unaona sasa mimi toka jana nimekuambia wazazi wako bado wana wasiwasi na wewe mshukuru sana huyo housegirl wenu kakusaidia sana asingetumia huo ujanja sijui ingekuwaje" Maria:  "huyu housegirl wetu mtoto wa mjini ndio maana nampenda hata mlinzi wetu pia mjanja mpenzi kwa hiyo wala usiogope hakiharibiki kitu" Johnson:  "poa mpenzi fanya kama nilivyokuambia ukipata muda mzuri uje huku gengeni kwangu umsikilize mzee Joseph anataka kukuambia nini" Johnson alimaliza kuongea na Maria akakata simu, muda huo huo akamfuata mzee Joseph kwenye kiduka chake. Wakasalimiana pale wakataniana kidogo kama kawaida yao mzee Joseph akamtania Johnson akamwambia "we kijana safari hii lazima nikuibie yule mtoto yani wewe una msichana kwao wana mapesa vile halafu hadi leo unauza hicho kigenge chako ngoja wajanja tumuibe uone tunavyomtumia vizuri" Johnson alicheka sana kusikia yale maneno ya mzee Joseph akamwambia "we mzee ushazeeka sasa hivi hayo mambo tuachie vijana kwanza huwezi kumuiba yule mtoto hapa amefika hasikii wala haoni mimi namkuna vizuri ndio maana kadata sasa wewe mzee utampa raha gani mtoto mbichi kama yule" Mzee Joseph:  "we kijana ng'ombe hazeeki maini mimi nikimchukua yule kwako harudi tena anakusahau'’ Mzee Joseph na Johnson walitaniana pale wakacheka sana Johnson akaanza kumuelezea yule mzee kilichompeleka pale. Akamuambia Mzee yule msichana wangu jana kaja kulala kwangu leo asubuhi wakati namsindikiza nikakumbuka yale maneno uliyoniambia siku ile kuwa nimjaribu nimuombe aniongezee mtaji mimi nimeogopa kumuambia hilo swala kwa hiyo nimemwambia akipata muda aje hapa gengeni kwangu ili niongee naye hilo swala wakati na wewe upo unisaidie kumpa maneno hadi aelewe. Mzee Joseph alimsikiliza Johnson kwa makini akamuambia "we kijana muoga sana unamuogopa hadi mpenzi wako wakati kila siku mnavuliana nguo haina shida ngoja aje tujaribu kumpanga kama ataelewa ila mchongo ukiwa poa lazima unipe na mimi mzee wako pesa ya pombe" Johnson akacheka akamwambia "usijali mzee mimi na wewe tena nakukubali sana mzee wangu" Wakati Johnson anaongea na mzee Joseph simu yake ikawa inaita kucheki alikuwa ni Maria akapokea lakini akashangaa kumsikia Maria analia kwenye simu
Itaendelea………………………..

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top