ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5



Ilipoishia
Maria alitoa mfuko uliokuwa na chips kuku akampa Johnson akamuambia asihangaike kupika. Johnson alifurahi sana akamtania Maria akamwambia "sijui kama siku nikiwa jela utaniletea vitu kama hivyo"


Endelea
Maria: usiseme hivyo mpenzi wangu nani ambaye atakupeleka jela sasa? Johnson: kwani wewe umesahau wazazi wako walisema siku wakigundua kuwa mimi na wewe bado tuna mahusiano watanifunga au watanipoteza duniani? 
Maria: "usiogope mpenzi wangu vile vitisho tu mimi siwezi kukuacha hata wazazi wangu wafanye nini na siku wakikufanyia kitu kibaya tu basi mimi watanikosa naweza nikajiua kwa ajili yako" Johnson: "hayo maneno unaongea kwa vile tu tupo wote hapa siku mimi nikifa au nikifungwa utanisahau tu na utapata mwanaume mwingine sababu wazazi wako hawataki uwe na mtu kapuku kama mimi wanataka wakusomeshe uje uolewe na mtu mwenye pesa siyo mimi muuza genge" Machozi yalianza kumtoka Maria alivyosikia yale maneno ya Johnson akamwambia "Johnson baby usiongee maneno kama hayo mimi nakupenda wewe na hiyo hiyo hali yako uliyonayo na ukumbuke tumetoka mbali sana kwa hiyo mimi siwezi kukuacha hata iwaje" Johnson: "haya mpenzi si tupo tutaona tu mwisho wake utakuwaje tumuombe tu Mungu atusaidie" Johnson na Maria waliongea mengi sana hadi muda wa kulala ulivyofika wakalala zao. Saa 12 asubuhi kama kawaida Johson aliamka akaanza kujiandaa kwa ajili ya kuwahi gengeni kwake akamuamsha na Maria. Mpenzi amka ujiandae uwahi kwenu kumbuka leo wazazi wako ndio wanarudi safari wasije wakakukosa wakatuletea balaa. Maria: "baby wewe wahi tu mimi niache nipumzike kidogo nitaamka saa nne ndo nitaenda nyumbani siwezi kuwahi asubuhi yote hii" Johnson: "siwezi kuondoka na kukuacha wewe hapa kwangu nitakuwa sina amani nitakaa kwa wasiwasi we amka ujiandae utaenda kupumzika hata kwenu" Johnson na Maria walibishana sana lakini mwisho Maria alikubaliana na mpenzi wake akamka akajiandaa wakatoka wote pamoja wakawa wanaelekea kwenye kituo cha daladala. Wakati wapo njiani wanapiga stori zao Johnson akakumbuka yale maneno ya mzee Joseph aliyomuambia kuwa akimtumia vizuri Maria anaweza akamtoa kimaisha. Johnson: "Mpenzi nimekumbuka kitu yule mzee wa kule gengeni kwangu jana aliniambia anataka kuongea na sisi kwa hiyo ukipata muda uje kule gengeni kwangu tumsikilize anasemaje" Maria: "sawa mpenzi wangu lazima nikipata muda nije yule mzee tangu siku ile atupatanishe na kutuambia yale maneno nimetokea kumpenda sana na kumuheshimu." Maria hakujua kuwa Johnson alitaka kumpambanisha kwa yule mzee ili ampange aanza kumpa pesa za kuendeshea biashara zake, wakati Johnson na Maria wapo kwenye kituo cha daladala wanaendelea kuongea simu ya Maria ikaita kucheki alikuwa ni mama yake Maria alistuka sana akajua tayari wazazi wake tayari wameshafika nyumbani kwao ndio maana wanampigia simu. Alipokea ile simu wakasalimiana na mama yake mama yake akamwambia "mwanangu Maria mwambie housegirl atuandalie chakula kizuri tupo njiani tunarudi tuna njaa sana"
Maria: "sawa mama namwambia mtakuta tumewaandalia chakula kizuri." Wazazi wa Maria hawakujua kuwa muda huo wanapiga simu Maria yupo na Johnson walijua kalala nyumbani Johnson alichanganyikiwa Maria alivyomwambia zile habari kuhusu ile simu aliyopigiwa, hakutaka kupoteza muda akaita bodaboda Maria akapanda akaondoka zake, Johnson akapanda daladala safari ya kwenda gengeni kwake ikaanza huku akimuomba Mungu Maria afike haraka nyumbani kwao kabla wazazi wake hawajafika.
Itaendelea............

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top