Salum Madadi (pichani kushoto)
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Salum Madadi kuwa Mkurugenzi
wake mpya wa Ufundi. Uteuzi huo umefanya na Kamati ya Utendaji katika kikao chake cha dharura kilichofanyika jana (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Kabla ya uteuzi, Madadi alikuwa akikaimu nafasi hiyo tangu Januari mwaka huu baada ya Mkurugenzi wa Ufundi aliyekuwepo kumaliza mkataba wake Desemba 31 mwaka jana. Madadi mwenye leseni A ya ukocha ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni kocha mwenye uzoezi wa zaidi ya miaka 30 ambapo alianza kufundisha mpira wa miguu mwaka 1980 katika klabu ya Maji SC ya Lindi.
Ana elimu ya sekondari aliyoipata katika shule ya Chidya na diploma ya ukocha wa mpira wa miguu aliyoipata nchini Ujerumani. Pia ni Mkufunzi wa makocha wa CAF, na alijiunga na TFF mwaka 2006 akiwa Ofisa Maendeleo. Alikuwa Kocha wa Taifa Stars mwaka 2000. Mbali ya Maji SC, amewahi kufundisha timu za Nyota Nyekundu, Ushirika ya Moshi, Simba, Shangani ya Zanzibar, Malindi ya Zanzibar, Cardif ya Mtwara na Kariakoo ya Lindi. Pia amewahi kuwa mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Slider[Style1]
Style2
Style3[OneLeft]
Style3[OneRight]
Style4
Style5
Tagged with: Michezo
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
- Popular Post
- Video
- Category
Películas populares
-
Simulizi kali ya kutisha iliyoandikwa na Amir Malick, imeanza leo sehemu ya kwanza...
-
ILIPOISHIA: “MAMAA.. MAMAAAAAAAAAAAAA….!!!” Kelele zilisikika kutoka ndani ali...
-
ILIPOISHIA: Macho yalikuwa yamebadirika rangi na kuwa myekunduuu kama amemwagiwa maji ya p...
-
MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA III – (NAFASI 100) Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
-
Ilipoishia Maria alimpigia Johnson simu akamwambia anataka akalale tena nyumbani kwake Johnson akamgomea akamwambia asije sababu waz...
-
COMPUTER SYSTEM ANALYST II (MOBILE APPLICATIONS DEVELOPMENT/PROGRAMMER) POSITION DESCRIPTION: COMPUTER SYSTEM ANALYST II (...
-
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte) limesema kuanzia mwaka huu wa masomo, wanafunzi wanaotaka kujiunga na masomo ngazi ya astasha...
-
Ilipoishia Mzee Joseph akamuambia Maria "Binti umependeza sana we mrembo kweli Johnson anajua kuchagua" Maria akacheka kusikia...
-
The Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) is focusing on increasing the outreach and service quality of its Energy products f...
-
Ilipoishia Johnson alipanga kumpa Maria penzi zito ile siku sababu alimfurahisha sana
No comments: