ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5



Ilipoishia
Johnson alifika kazini kwake kama kawaida alifanya usafi alipanga vitu vyake mara akaona gari aina ya Noah imepaki mbele ya genge lake alijua ni wateja akaenda kuwasikiliza vioo vya gari vilifunguliwa Johnson hakuamini macho yake ndani ya gari alikuwa ni Mama na Baba yake Maria...
Endelea
Johnson alishtuka sana ilibaki kidogo akimbie akajua mambo yameshaharibika alivyomlaza Maria nyumbani kwake mapigo yake ya moyo yalianza kwenda mbio huku anatetemeka Akawasalimia wazazi wake Maria lakini hawakuitikia wakawa wanamuangalia kwa hasira Mama yake Maria akamuambia Johnson "Hatuna shida na salamu yako tunachotaka utuambie binti yetu sehemu alipo tangu jana aende chuo hadi muda huu hajarudi nyumbani tunajua wewe ndo unajua sehemu alipo" Johnson akamjibu "Mama mimi sijui chochote mimi nina muda mrefu sijaonana na Maria labda kuna mahali yupo ila mimi sijui chochote" Baba yake Maria akamwambia "Sikia we kijana sisi sio watoto wadogo wewe ndo unayefanya binti yetu asisome wewe ndIo unayefanya binti yetu asikalike nyumbani sasa hivi umefikia hatua ya kumlaza nje kama mke wako tuambie haraka binti sehemu ulipomuweka kabla sijakufanyia kitu kibaya" Baba yake Maria akashuka ndani ya gari akamfwata Johnson akamkunja watu walijaa sana pale gengeni kwa Johnson kuangalia kile kilichotokea Johnson alijisikia aibu sana lakini alionyesha ujasiri wake alikataa kabisa kuwa hajui Maria sehemu aliyolala lakini pia alijiuliza Maria atakuwa kaelekea wapi wakati asubuhi waliachana pale nyumbani kwake yeye akawa anakuja gengeni kwake Maria akawa anaelekea nyumbani kwao Johnson alijuta kumkubalia Maria kulala nyumbani kwake kwa kile kichomtokea pale gengeni kwake wazazi wake Maria walivyoona Johnson anaendelea kubisha wakamwambia "Hebu funga kigenge chako tupeleke unapoishi tukaangalie kama kweli binti yetu haupo naye" Johnson alifunga genge lake haraka akapanda kwenye gari safari ya kuelekea kwake ikaanza Alijawa sana na wasiwasi akawa anawaza isije ikawa Maria aliogopa kwenda nyumbani kwao akawa amerudi nyumbani kwa Johnson tena akajua ikiwa hivyo na wazazi wa Maria wakimkuta binti yao kwake ndo utakuwa mwisho wake Wakati wapo njiani ndani ya gari wazazi wa Maria walikuwa wanamtukana sana Johson na kumtolea maneno makali ya dharau hadi Johnson alijisikia vibaya machozi yakawa yanamtoka Baba yake Maria akamuambia Johnson "yani kijana tukimkuta binti yetu huko kwako ndo utakuwa mwisho wa maisha yako sisi tumeacha kazi zetu tunasumbuliwa na kijana mdogo kama wewe hatuwezi kukubali binti yetu achezewe na maskini kama wewe usiye na mbele wala nyuma" Yale maneno yalimuumiza sana Johnson hadi alijuta kuanza mahusiano na Maria
Itaendelea..........

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top