Manchester City imejikuta katika wakati mgumu usiku huu baada ya kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Sunderland Uwanja wa Etihad.
Fernandinho alitangulia kuifungia Manchester City dakika ya pili akimalizia pasi ya Sergio Aguero, lakini kinda wa umri wa miaka 21 wa England, Connor Wickham akaisawazishia Sunderland dakika ya 73 kwa pasi ya Mtaliano Emanuele Giaccherini.
Wickham akaifungia bao la pili Sunderland dakika ya 83 kwa pasi ya Giaccherini tena, lakini Mfaransa Samir Nasri akainusuru City kuzama kwa kuisawazishia dakika ya 88 kwa pasi ya Jovetic.

No comments: