ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5

KING MAJUTO APIGA TAFU KITUO CHA POLISI MJIMWEMA


Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akizungumza jambo wakati wa hafla ya kupokea Vifaa vya Solar kutoka kampuni ya Steps Solar kwa ajili ya Kituo cha Polisi cha Polisi cha Mjimwema,Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Solar,Dilesh Solank.

CLOUDS MEDIA YAPATA LESENI YA URUSHAJI MATANGAZO NCHI ZA FALME ZA KIARABU



Kampuni ya Clouds Media International leo imetangaza kuwa imepewa leseni ya kurusha  matangazo  katika nchi za umoja wa falme za kiarabu (UAE).  Akielezea kuhusu leseni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni  hiyo Bwana Joseph Kusaga, amesema  sasa kituo cha  Clouds TV kimataifa kitakuwa kikishuhudiwa na watu wa mataifa mbalimbali.

Clouds TV kimataifa ni mwendelezo wa televisheni maarufu sana kwa vijana  nchini Tanzania,  hata hivyo sehemu kubwa ya maudhui yatakayokuwemo kwenye Clouds TV kimataifa itakuwa na mpangilio mpana wa vipindi kwa watazamaji vitakavyorushwa kwa  lugha za Kiingereza na Kifaransa. Akieleza zaidi Kusaga amesema "Leo ni siku ya  kihistoria na alama ya hatua moja katika mpango wetu wa kina wa kupeleka maudhui ya Clouds TV kimataifa kupitia  matangazo kwa njia ya  mitandao’’.

Clouds TV kimataifa  haitotoa tu burudani, lakini pia itakuwa kiunganishi kwa waafrika waishio katika umoja wa nchi za falme za kiarabu pamoja na kuwapa fursa za kutangaza bidhaa zao na kuimarisha uhusiano baina yao.

LADY JAY DEE AFUNIKA SHOW YAKE YA NYUMBANI LOUNGE ACHA KABISA

IMG_4930 IMG_4931

P-FUNK AUKACHA UBACHELA, UFUNGA NDOA JIJINI ARUSHA

Mtayarishaji wa Muziki ambaye ni mmiliki wa Bongo Records, P-Funk Majani amefunga ndoa na mrembo aitwaye Hidaya. Wawili hao wamefunga pingu za maisha jijini Arusha.

VIDEO YA WEUSI 'GERE' KUACHIWA WIKI IJAYO

Gere video3Zile teaser za Weusi zilizokuwa na title ya ‘OTEA’ ambazo wamekuwa wakiziweka kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii kuanzia wiki iliyopita, tayari imefahamika kuwa ni ujio wa
video ya single yao mpya
"Gere".

SKYLIGHT BAND WAFANYA UZINDUZI RASMI WA NYIMBO MPYA YA 'KARIAKOO' PAMOJA NA KUTAMBULISHA STUDIO YAO


Meneja wa Band ya Skylight Aneth Kushaba akielezea kwa kina uzinduzi Rasmi wa wimbo wao Mpya unaokwenda kwa jina la Kariakoo ambapo uzinduzi huo uliambatana na Video pamoja na Audio. Pia ametambulisha Rasmi Studio ya kurekodi Muziki ambapo sasa nyimbo zao watakuwa wanafanyia katika Studio yao.

Kutoka kushoto ni mmoja wa waimbaji wa Skylight Band Sam Mapenzi, wakatikati ni Meneja wa Band hiyo Aneth Kushaba pamoja na Mwimbaji mwengine wa Skylight Band Joniko Flower wakiwa wanazungumza na waandishi wa Habari na wadau mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa wimbo wao mpya wa Kariakoo pamoja na Kutambulisha Rasmi Studio yao

AFRICAN STARS 'TWANGA PEPETA' WAINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA PROIN PROMOTIONS KUANDAA KAZI ZAO


Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka, alisema mkataba huo una manufaa kwa bendi hiyo kutokana na kutaka kuwanufaisha wanamuziki na wasanii wa nchini kwa ujumla.

SHINDANO LA KUSAKA VIPAJI VYA UIGIZAJI TANZANIA MOVIE KWA KANDA YA ZIWA KUMALIZIKA LEO

Majaji wa Shindano la Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents, Single Mtambalike (kulia), Yvonne Chery (Katikati) na Roy Sarungi (Kushoto) wakipitia alama za washiriki kwaajili ya kuweza kuwatangaza washindi waliofanikiwa kuingia hatua ya tatu ambapo wanachukuliwa washiriki 30 kwaajili ya kupata mchujo wa washindi watatu bora ambao wataibuka na Kitita Cha Shilingi laki 5 kila Mmoja kwa Kanda ya Ziwa na baadae kujiunga na washindi wengine watatu kutoka kila kanda katika fainali ya mwisho itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam na Mshindi Kujinyakulia Zawadi Kubwa kabisa ya Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania. (50,000,000/=)
⬆
Top