Thursday, June 05, 2025

ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  Mtendaji Mkuu wa kampuni ya UNHWA ya Jamhuri ya Korea Kusini  Bw. Young Woo Jin na ujumbe wake na uongozi wa NIMR walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa NIMR Dk. Mwele Malecela.



Taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu Tanzania (NIMR), imesaini mkataba wa ushirikiano na kampuni ya UNHWA ya Jamhuri ya Korea Kusini ambapo kampuni hiyo itaisaidia NIMR teknolojia mpya ya kufanya ugunduzi wa dawa za binadamu kwa kutumia mimea.

Makubaliano hayo yamesainiwa jijini Dar es salaam pembezoni mwa kongamano la 28 la kisayansi la NIMR, ambapo mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo Dk. Mwele Malecela amesema hatua hiyo ni muhimu katika shughuli za utafiti wa afya nchini na maendeleo ya taasisi kwa ujumla.

Dk. Mwele amesema teknolojia hiyo itaongeza uwezo wa kiwanda cha taasisi cha kutengeneza dawa kwa kutumia mimea kilichopo eneo la Mabibo External jijini Dar es salaam na kwamba itawezesha taasisi kujikita zaidi katika utengenezaji wa dawa za saratani mbalimbali pamoja na za kusaidia udhibiti wa virusi vya ukimwi.

Kwa upande wake afisa mtendaji mkuu wa kampuni hiyo ya NHWA bw. YOUNG WOO JIN amesema kampuni yake imefikia hatua hiyo kutokana na mchango wa NIMR katika masuala ya tafiti na ugunduzi wa dawa ambapo ameahidi kuendelea kushirikiana na taasisi hiyo katika kiteknolojia ili kuiongezea uwezo.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
JOHNSON NA MARIA
»
Previous
AJIRA: NAFASI ZA KAZI KUTOKA SUMATRA

No comments:

Post a Comment


Top