ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5


 Tingatinga la Mamlaka ya Ustawishaji makao makuu [CDA] likibomoa moja ya
nyumba zilizopo katika hifadhi ya Barabara inayotarajiwa kuanza
kujengwa havi karibuni, ambapo zaidi ya nyumba 65 zilibomolewa katika
eneo hilo la mlamwa kusini.
 Wanawake wa mtaa wa Mlimwa wakimsaidia Mwenzao aiyezilai baada ya
Tingatinga la CDA kufika kwa ajili ya kubomoa nyumba yake kwa ajili ya
kupisha ujenzi wa Barabara, zoezi hilo lilifanyika Jana ambapo nyumba
zaidi ya 65 zilibomolewa na kuacha familia zaidi ya 150 zikikosa makazi.
 Mwenyekiti wa mtaa huo Zubeda Haji akielekeza jambo wakati wa ubomoaji huo.
 Wananchi wa Mlimwa waking’oa mabati muda mfupi kabla ya Tinga tinga la
CDA kufika na kuibomoa nyumba hiyo ili kupisha hifadhi ya Barabara

Bibi huyu mkazi wa Mlimwa Kusini ambaye hakufahamika jina lake akiwa
hajui la kufanya baada ya nyumba yake aliyokuwa akiishi iliyojengwa kwa
mtindo wa Tembe huku akiachwa na vyombo vyake alivyoweka kwenye shamba
la mahindi baada ya CDA kufanya uvunjaji huo kwa nyumba zote zilizopo
katika hifadhi ya Barabara.
Wananchi wa Mlimwa kusini wakiwa katika hekaheka ya kuhamisha mizigo yao
na kukimbia nyumba zao baada ya kupata taarifa za ujio wa Tinga tinga
la CDA kwa ajili ya kubomoa nyumba zao ili kupisha ujenzi wa barabara.
PICHA NA JOHN BANDA WA PAMOJA BLOG

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top