Hii imetokea huko Ufarasa baada ya John Dowling (58) na mwanae Rob (23)kuanza
kushindana kuserereka kwenye barafu, mchezo ambao upendwa sana nchini
Ufaransa, Baba huyo na mwanae walitumia kiwanja cha barafu ambacho
kilikua kinaandaliwa kwa ajili ya mashindano siku inayofata, huku ikiwa
imewekwa mageti special ili watu wasipite kwa kuwa uwanja ulikiua kwenye
maandalizi.

Hapo ndipo alipo anguka na kujigonga kwenye Geti hilo la Chuma


Mtoto
huyo aliweza kumpita baba yake, huku baba huyo akijaribu kuongeza
mwendo ili amfikie mwanae kwa bahati mbaya akatereza vibaya na kuanguka
na kujigonga kwenye geti na kumfanya damu nyingi kuanza kumtoka kichani
kwake.

Akiwa anaangaliwa huku wakiwa wanasubiri usafiri kuja kumchukua kumpeleka hospitalini
"Baada
ya baba kuanguka nilijua kaumia na alianza kupiga makelele sana,
nikajua ameumia vibaya ikanibidi nimsaidie kumtoa, alivyopelekwa
Hospitali nilibaki nafikiria nikikumbuka kilichomtokea Michael Schumacher, sikujua
kama atakufa au atapona, ila nikashangaa baada ya siku tatu amepona na
kurudi kwenye kutereza tena kwa spidi." alisema mwanae Rob

Baba huyo akiwa anapelekwa Hospitali ambapo alitibiwa kwa siku tatu na kuruhusiwa kutoka
No comments: