Usijali machozi yanayoletwa na
vitunguu, vitunguu ni kama karata dume
katika kupigana na magonjwa. Ni mmea
mahiri katika familia ya lily, vinakupa
faida nyingi kiafya pia yaongeza ladha
nzuri katika chakula chako.
Tuangalia haraka haraka faida
zitokanazo na kula vitunguu maji.
1. Vina kemikali ambazo
zinasaidia kazi ya Vitamini C katika
mwili wako, hivyo kukuongezea kinga
ya mwili.
2. Vina kemikali aina ya
chromium ambayo inasaidia
kudhibiti sukari katika damu.
3. Kwa karne nyingi, vitunguu
vimekuwa vikitumika kupunguza
uvimbe na kuponya maambukizi.
4. Unafurahia vitunguu vilivyokatwa
kwenye chakula? Kama ndio basi
furahi! Vitunguu vibichi vinasaidia
kutegeneza cholesterol nzuri (HDL)
hivyo kuufanya moyo wako kuwa na
afya njema.
5. Kemikali yenye nguvu iitwa
quercetin katika vitunguu
inatambulika kwa kusaidia kwa kiasi
kikubwa kuzuia saratani (cancer).
6. Umeumwa na nyuki? Weka juice ya
kitunguu eneo ambalo umeumwa
upate nafuu ya maumivu na uvimbe
kutowasha.
7. Vinasaidia kuzuia vidonda
vya tumbo.
8. Sehemu ya kijani (kitunguu kutoka
shambani) imejaa Vitamini A
kwahiyo itumie mara kwa mara.
FAIDA NANE ZA VITUNGUU MAJI

No comments: