HIVI PUNDE: MKUU WA MKOA WA MARA AFARIKI GHAFLA
Habari za hivi punde zinasema kuwa, John Tupa, Mkuu wa Mkoa wa Mara, (pichani) amefariki ghafla muda mchache uliopita. Kwa mujibu wa mtoa habari ni kuwa marehemu Tupa, alikuwa akitoka katika moja ya kikao cha utendaji mkoani kwake ambapo baada ya kupewa 'Breafing', sasa alikuwa akielekea eneo husika kwa ajili ya kutembelea na kukagua kile alichoeleza katika taarifa hiyo, na wakati akipanda gari ndipo alipoanguka na kupoteza maisha.

No comments: