ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5

                                     
                           Hizi ndizo mpya za msimu ujao za Manchester United?

Jezi mpya za Mashetani Wekundu zimevuja kwenye mitandao ya kijamii, ambazo ni za Nike zikiwa na rangi nyekundu na chata la rangi nyeupe wadhamini wapya, Chevrolet kwa mbele.
Jezi hizo zina zipu nyeusi kutokea shingoni kuelekea chini na ufito mweusi kwenye pindo za mikono na mabegani.
Pamoja na hayo haijathibishwa kama habari kuhusu jezi hizo ni sahihi. United ilitangaza Julai mwaka 2012 udhamini wa jezi na Chevrolet, ambao watakuwa wakilipa Pauni Milioni 25 kwa mwaka kuweka jina lao kwenye jezi za timu hiyo kuanzia msimu ujao.
Wadhamini wa sasa wa United, Aon, hawataonekana tena kwenye jezi za timu hiyo kuanzia msimu ujao.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England wanaweza kuvuna fedha zaidi kutokana na ongezeko la dau la udhamini wa vifaa vya michezo. United imekuwa kwenye mazungumzo na Nike kuingia Mkataba wao mpya wa miaka 13, lakini kwa mujibu wa Daily Mail, Wekundu hao wanajiandaa kuingia kwenye miezi mingine sita ya kusaka dili zuri zaidi kabla ya kujitia pingu. Mkataba wa sasa wa Nike unamalizika mwishoni mwa msimu ujao.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top