ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5

Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera akiendesha kikao cha Kamati ya Uchumi na Fedha cha Halmashauri ya Mji kujadili mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Pembeni ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji ambaye ni Diwani wa Kata ya Mtonga, Mheshimiwa Francis Komba (kushoto), anayefuatia ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Dokta Jerry Mwakanyamale (kulia) na Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto).
Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto) akieleza umuhimu wa matumizi ya Tiba kwa Kadi (TIKA) kikao cha Kamati ya Uchumi na Fedha cha Halmashauri ya Mji kujadili mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Kikao hicho cha tatu kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Pembeni ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Dokata Jerry Mwakanyamale (kulia), Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji ambaye ni Diwani wa Kata ya Mtonga, Mheshimiwa Francis Komba.
Wajumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha ya Halmashauri ya Mji Korogwe, Tanga wajadiliana jambo wakati wa kikao.
Diwani wa Kata ya Kwamdolwa, Mheshimiwa Hillary Ngonyani akijadili jambo.
Mchumi wa Halmashauri ya Mji Korogwe, Bw. Kikonge Jeremiah akitoa tathimini zake juu ya matumizi ya Tiba Kwa Kadi (TIKA) kwa wananchi wa halmashauri yao.
Diwani wa Kata ya Ngombezi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya, Maji na Uchumi, Mheshimiwa Omari Chafesi akitoa mwongozo na mtazamo wake katika mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA).
Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji Korogwe, Rabeca Balisidya (wa kwanza kulia) kitoa ufafanuzi wa vifungo vya sheria katika mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Pembeni yake ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Dokta Jerry Mwakanyamale na Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera.
Afisa Muuguzi Kitengo Cha Afya ya Akili, Ayubu Mwakalila nae hakuwa nyuma kutoa mtazamo wake juu ya mada iliyokuwa ikijadiliwa.
 
Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top