Kundi la muziki kutoka mjini Morogoro Team Recers ambalo
linaundwa na wakali kama Rota, Kacci, Raid, Concious, Big Poppa na producer wao wa
audio na video GQ
Team Recers walisema ”Ebwana tumepata dili safi
yani naweza kusema hii ni moja kati ya hatua kubwa tuliyopiga na hii yote ni
kwaajili ya kazi nzuri pamoja na nidhamu tulionayo. Team Racers
imesaini mkataba na kampuni ya maziwa inayoitwa LEWIS MTINDI BORA ya
mjini Morogoro.
Katika mazungumzo baina ya msemaji mkuu wa Team Racers na Mkurugenzi
wa kampuni hiyo Mr Urio makubaliano ambayo yamewekwa ni kuwa members wa Team Racers wanakuwa mabalozi wa product hiyo ikiwa ni kufanya matangazo pamoja na
kupromote product hiyo ya maziwa. Kiukweli imetuzidishia juhudi ya kuendelea
kufanya kazi vizuri zaidi.
No comments: