
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi
akizindua mradi wa maji kwenye kijiji cha Chididimo Manispaa ya Dodoma, wengine ni wajumbe wa chombo huru cha watumiaji maji kijijini
hapo.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwasha
mashine ya kusukuma maji kwenye mradi wa maji kijiji cha Chididimo Manispaa ya Dodoma baada ya kuzindua mradi huo.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi
(kushoto) akizungumza na viongozi pamoja na wananchi wa kijiji cha Chididimo kilichopo
manispaa ya Dodoma kuulinda na kuutunza mradi wa maji kijijini hapo mara baada ya mkuu huyo wa mkoa kuuzindua mradi huo.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi
(kulia) na katibu tawala Mkoa
Dodoma Ndg. Rehema Madenge wakifungua na kukinga maji kwenye mradi wa
maji kijiji cha Chididimo kilichopo manispaa ya Dodoma wakati wa uzinduzi wa mradi
huo. Wanaoshuhudia ni wananchi wa kijiji cha Chididimo.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi
akimtwika
ndoo ya maji mdala Morleni Mwaluko mmoja wa Wanakijiji cha Chididimo,
maji hayo safi kwa sasa yanapatikana kwa urahisi na kwa karibu
kijijini hapo baada ya kukamilika kwa mradi wa maji wa kijiji hicho,
mkuu wa Mkoa Dodoma amezindua mradi huo.

Mkuu
wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akisalimiana na wanafunzi wa shule
ya msingi Chididimo waliojitokeza kumlaki alipowasili Kijijini hapo
kuzindua mradi.

Mkuu
wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi(kushoto) akipokea taarifa ya mradi
wa maji kijiji cha Chididimo Manispaa ya Dodoma kama inavyowasilishwa
kwake na mhandisi Mohamed Khali (kulia) kutoka idara ya maji Manispaa
ya Dodoma wakati wa sherehe ya uzinduzi.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi
(aliyeshika kibuyu katikati) akiimba na kuserebuka nyimbo za asili ya
kigogo pamoja na akinamama wa kijiji cha Chididimo Manispaa ya Dodoma
kusherehekea baada ya mkuu huyo wa mkoa kuzindua mradi wa
maji kijijini hapo.
No comments: