Friday, June 06, 2025

ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5

P1130382
Afisa habari kitengo cha habari Umoja wa mataifa nchini Tanzania(UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza katika viwanja vya Mazingira Senta mjini Shinyanga kwenye warsha ya siku moja iliyokutanisha shule 10 za sekondari, vyuo na walimu kutoka katika shule na vyuo hivyo vilivyopo katika manispaa ya Shinyanga, ambapo alisema Umoja wa Mataifa(UN) unalipa suala la elimu kipaumbele sana kwa wanafunzi hivyo kuwataka wanafunzi kuwa na malengo katika maisha yao kwa kusoma kwa bidii,kuepuka vishawishi vinavyopelekea kupata ujauzito wakiwa wanafunzi tena chini ya umri wa miaka 18.

Afisa habari huyo pia aLItumia fursa hiyo kuwatahadharisha wanafunzi wa kike kuepuka ngono kwani kwa mujibu wa utafiti wao takwimu zinaonesha kuwa vijana wa kike wenye umri wa miaka 15-19 wana uhusiano wa kingono na wanaume wanaowazidi miaka juu zaidi ya umri wao hivyo kuwepo kwa hatari ya kuambukizwa VVU na Mimba za utotoni.Kushoto ni Mwenyekiti wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA) tawi la Shinyanga bwana Ezra Manjerenga.
100_5397
Wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari Busurwa, Uhuru, Mazinge, Buluba, Chamaguha, Kizumbi, wakimsikiliza Afisa habari kitengo cha habari Umoja wa mataifa nchini Tanzania (UNIC) Bi Usia Nkhoma Ledama (hayupo pichani) ambaye alisema kwa mujibu wa sensa yao mwaka 2012 asilimia 65 ya Watanzania wote vijana wenye umri wa miaka chini ya 24,lakini pia asilimia 40 ya vijana wa kike wenye miaka chini ya 18 wanapata mimba za utotoni na wengine kuolewa katika umri huo.Aliongeza kuwa asilimia 23 ya vijana umri wa miaka 15-19 wameanza kuzaa na katika umri huo kati ya vijana wanne basi mmoja anaolewa ama kupata mimba.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UJERUMANI DKT FRANK-WALTER STEIMEIER IKULU DAR
»
Previous
MATOKEO CRICKET

No comments:

Post a Comment


Top