ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5



Mratibu wa Kupinga Vitendo vya ukatili wa Kijinsia wa Walter Reed Program, Thorm Chacha wakati wa Semina kwa waandishi wa habari iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Mbeya Peak.



Makamu mwenyekiti wa Clabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Mbeya Modestus Mkulu akifungua Semina hiyo





                   Gabriel Mbwile moja kati ya wawezeshaji katika semina hiyo


           Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Mbeya wakiwa katika semina hiyo









Vitendo vya ukatili wa kijinsia ni moja ya sababu iliyochangia ongezeko la maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika Mikoa ya Kanda ya Nyanda za juu kusini.
Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Kupinga Vitendo vya ukatili wa Kijinsia wa Walter Reed Program, Thorm Chacha wakati wa Semina kwa waandishi wa habari iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Mbeya Peak iliyopo jijini hapa.
Alisema sababu hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Shirika la Walter Reed Programu kwa Kushirikiana na Shirika la Henry Jackson For Medical Research la Marekani ambao unaonesha ukatili wa kijinsia ndani ya familia na Kaya huchangia maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Chacha alibainisha kuwa utafiti umeonesha kuwa tabia za wanaume kukwepa majukumu yao ndiyo kiini cha tatizo ya kuongezeka kwa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na kuchangia kuongezeka kwa maambukizi mapya.
Alisema vitendo vya ukatili vinavyofanywa na wanaume ni pamoja na kutelekeza familia zao hali ambayo imesababisha watoto kutopata malezi ya wazazi wote na hivyo wanajikuta wakiwa katika mazingira hatarishi pindi ndoa zinapovunjika na familia kusambaratika.
Alisema ipo haja kwa mashirika yanayojishughulisha na kupinga vitendo vya ukatili nchini kuweka nguvu zaidi maeneo ya vijijini,maeneo ambayo wanawake wameachiwa mzigo mkubwa wa kulea familia.

Aliongeza kuwa katika kukabiliana na ongezeko la maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi serikali na wadau pamoja na wananchi kwa ujumla mkoani Mbeya wanapaswa kusimamia ipasavyo sheria zilizopo dhidi ya watu wanaodaiwa kufanya ukatili wa kijinsia.
Alisema ili kuhakikisha ukatili wa kijinsia na maambukizi ya ukimwi yanapungua shirika hilo limeanzisha vituo vya kushughulikia ndani ya Mkoa wa Mbeya ambavyo viko katika Wilaya 6, kata 27 na vijiji 121 pamoja na Jiji la Mbeya.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top