Kituo cha afya cha Ikonongo kilichopo kata ya Salawe wilayani
Shinyanga kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa
huduma ya maji na nishati ya umeme hali ambayo inawalazimu akina mama
wajawazito kutumia tochi ya simu au taa wakati wa kujifungua huku
watoto wanaougua kuchanganywa na wakubwa.Baadhi ya wananchi wa kata hiyo walieleza kuwa kumekuwepo na tatizo la kupata huduma iliyo bora kwani vifaa vya kupimia maradhi yanayowasumbua hakuna, mama wajawazito kutumia mwanga wa simu ya tochi wakati wa kujifungua , wamalizapo kujifungua nguo zao hulazimika kwenda kufulia kwenye malambo sehemu ambayo maji hutumiwa na watu wote.
Walisema wamekuwa wakipata shida ya kupata huduma katika kituo hicho kwani hakuna maji hivyo wanapokwenda kujifungua hulazimika kwenda na maji yao.
Mwenyekiti wa kijiji cha Azimio Twiga Mashimba alisema kuwa kituo hicho kinahudumia vijiji zaidi ya vitano na kata nne ambazo ni Mwakitolyo,Mwenge na Salawe ambapo kijiji chake kina watu zaidi ya 3000 na kwamba kituo kinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa wodi ya watoto ambao hulazimika kuchanganywa na wakubwa, kina mama hujifungua kwa kutumia mwanga wa simu ya tochi pia uhaba wa maji upo.
“ Kijiji hiki kinahudumia zaidi ya watu 21,000, awali kulikuwepo na sola ambayo ilikuwa ikisaidia kurahisisha huduma mbalimbali kwa wagonjwa lakini ilikwisha ibiwa na sasa hakuna sola vifaa vya kupimia maradhi mbalimbali ikiwemo malaria hakuna ,wodi ya kulaza watoto hakuna inawalazimu kuwachanganya na wakubwa hata wenye magonjwa ya kifua kikuu na kuhara”alisema .
Naye mkuu wa kituo hicho Dkt Saimon Wilson alisema vifaa vya kupimia baadhi ya maradhi vipo ila kuna wengine wagonjwa hulazimisha kupata vipimo vyote vingine havipo ila kwa upande wa kupima malaria kipimo kipo, suala la kujifungulia tochi ya simu sio kweli bali wanatumia taa ikiwa sola iliyopo haina nguvu na huzimishwa ifikapo saa tano usiku.
"Kituo hiki kinakabiliwa na changamto ya maji na nishati ya umeme, suala la sola kuibiwa siwezi kulizungumzia mimi nilikuta sola iliyopo na inatumika mpaka sasa ni hii nayo haina nguvu huwashwa na kuzimishwa saa tano usiku ,tunatumia taa za kawaida,pia wagonjwa kwa siku ni zaidi ya 80",aliongeza.
Diwani wa kata hiyo Joseph Budonho alisema kuwa kweli kituo hicho cha afya kina changamoto ya ukosefu wa nishati ya umeme na maji ila tatizo hilo linashughulikiwa ikiwa tayari nyaya za umeme zimekwisha wekwa isitoshe kuondoa tatizo la maji lililopo, kuhusu sola ilikuwepo zamani lakini iliibiwa na kesi bado ipo mahakamani.

No comments: