ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5

                                  DSC_0079

Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundi (Red Cross), Dr. George Nangale, akizindu rasmi kampeni ya ‘Save The Elephant’ (Okoa Tembo) kwa niaba ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kama jitihada za kumuunga mkono Rais Kikwete katika kupambana na ujangili wa wanyamapori nchini. Kushoto ni Mratibu wa Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania, Bw. Robert Zangi, Wa pili kushoto ni Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza, na Kulia ni Dr. Herry Muhando kutoka International Evangelist

Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania imezindua kampeni ya ‘Save The Elephant’ (Okoa Tembo) kama jitihada za kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete katika kupambana na ujangili wa wanyamapori nchini.

Mratibu wa taasisi hiyo, Robert Zangi, amesema wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwamba wameamua kumuunga mkono Rais Kikwete kutokana na kukithiri kwa matukio ya ujangili wa wanyamapori miaka ya hivi karibuni. Aliongeza kwamba kampeni hiyo itawalenga zaidi watu ambao wanaishi jirani na mbuga za wanyama.

“Watu wanaoishi jirani na mbuga za wanyama ni rahisi kufahamu nani ni jangili na nani ni raia mwema miongoni mwao,” alisema. Aliongeza kusema kwamba kampeni hiyo itawafikia watu wanaoishi jirani na mbuga za wanyama kwa lengo la kuwaelimisha umuhimu wa kupambana na jangili dhidi ya wanyamapori.                              DSC_0037
Mratibu wa Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania, Bw. Robert Zangi, akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Save The Elephant’ (Okoa Tembo) kupitia Taasisi yake kama jitihada za kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete katika kupambana na ujangili wa wanyamapori nchini. Wa pili kushoto ni Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza, Wa pili kulia ni Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundi (Red Cross), Dr. George Nangale (kwa niaba ya Rais Kikwete) na Kulia ni Dr. Herry Muhando kutoka International Evangelist.

Kampeni hiyo ina mpango wa miaka mitano ambao kwa kuanzia kutakuwa na matukio matatu makubwa mwaka huu kati ya sasa hivi na mwezi Mei.
Tukio la kwanza, alisema, ni la uzinduzi wa kampeni hiyo na la pili ni kuwasilisha ujumbe wa kampeni kwenye Umoja wa Mataifa nchini Marekani tarehe 9 mwezi Aprili na la tatu litakuwa ni semina juu ya kupambana na mauaji ya Tembo, Vifaru na wanyamapori wengine.
DSC_0030
Meneja Biashara wa Qatar Airways Tanzania, Bw. Basel Haydar (kushoto) pamoja na Meneja Mauzo wa Qatar Airways Tanzania, Bw. Emmanuel Okware.
DSC_0171
Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza akisisitiza jambo ambapo ametoa rai kwa wadau mbalimbali pamoja na mataifa mengine kuunga mkono jitihadi hizi kuhakikisha ujangili unatokomezwa.
Nae Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundi (Red Cross), Dr George Nangale, amesema kwamba wanaunga mkono kampeni hiyo kwani mauaji ya wanyamapori ni majanga na kwamba watu wanaoishi jirani ya mbuga za wanyama wanaweza kusaidia sana kwenye mapambano dhidi ya ujangili.
Nangale alikuwa anamwakilisha mgeni rasmi ambaye alikuwa awe Rais Kikwete.


Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza, alisema ni vizuri kuendelea kuwalinda Tembo na wanyamapori wengine na kuongeza kwamba kampeni hii ni muhimu sana na akaomba jitihada hizi ziungwe mkono na nchi jirani pamoja na mataifa mengine.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top