ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5



Matukio ya kukamatwa kwa Watanzania nchini China kwa kesi za biashara ya dawa za kulevya yana idadi kubwa sana ndani ya hii miaka mitano iliyopita.
Miezi miwili iliyopita Balozi wa Tanzania China alithibitisha kwenye kwamba Watanzania
 wasiozidi mia mbili ndio wamefungwa kwenye magereza mbalimbali ya China kutokana na kesi tofautitofauti ila dawa za kulevya ndio zinaongoza’
Balozi huyu alisema kwa wakati huo hakuwa na rekodi yoyote ya Mtanzania kuhukumiwa kunyongwa au yeyote ambae tayari ameshanyongwa na kwamba kwa taarifa zaidi Wizara ya mambo ya nje itafutwe.

Baada ya hayo yote, hatimae katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje John Haule March 25 2014 ametaja jumla ya Watanzania waliokamatwa kwa kesi ya dawa za kulevya kwa kusema‘tuna Watanzania wengi tu ambao wapo kwenye magereza kule China japo tumeshindwa kwa harakaharaka kupata idadi ya waliojihusisha na shughuli ya dawa za kulevya lakini kuna rekodi fupi tulizonazo sasa hivi’
Katika Magereza ya China mpaka February 2014, tumepewa taarifa na Mamlaka za China kwamba wapo Magerezani Watanzania 177 ambapo 15 kati yao wamehukumiwa kunyongwa kutokana na biashara hiyo ya dawa akini niseme tu wenzetu wa Serikali ya China wanatuthamini sana kama sisi tunavyowathamini’
‘Wenzetu wa China wanathamini zaidi uhusiano wetu na ndiyo maana hata wale wachache Watanzania waliohukumiwa kunyongwa hawajanyongwa mpaka leo na hatutegemei kama watanyongwa, yani sanasana watafungwa kifungo cha maisha gerezani’.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top