Klabu ya Atletico Madrid imeambulia sare ya 1-1 dhidi ya Barcelona katika nusu fainali ya kwanza. Hadi mapumziko hakuna aliyeona lango la mwenzake licha ya kosa kosa za hapa na pale.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na uliwachukua dakika 11 Atletico Madrid kushangalia goli la kutipia kwa Diego baada yakufumua shuti kali lililomshinda Pinto na mpira kujaa wavuni.
Baada yakupata bao hilo Barcelona walicharuka na kuliandama lango la Atletico na kuweza kusawazisha kupitia kwa Neymar dakika ya 71 kwa pasi murua ya Iniesta.
BARCA NA ATLETICO NGOMA DROO 1-1

No comments: