Afisa Mtendaji Mkuu wa BMTL, Copy Cat, Bw Mike Holtham akizungumza na mmoja wa wageni waalikwa katika sherehe hizo za kuzindua jina jipya nchini na kuzungumza na wateja wao.
.Yapata Afisa Mtendaji Mkuu Mpya
.yawa wakala rasmi wa bidhaa za Samsung Tanzania
Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
KAMPUNI
ya Business Machines Tanzania Limited (BMTL) imebadilisha rasmi jina
lake la biashara kwenda kwenye kampuni yake mama ya Copy Cat katika
harakati zake za kupanua wigo wa biashara nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni wakati wa
uzinduzi rasmi wa jina la biashara la Copy Cat nchini, Afisa Mtendaji
Mkuu Mpya wa Kampuni hiyo, Bw Mike Holtham amesema kampuni inayofuraha
ya kujiunga rasmi katika jina la kampuni mama ya makampuni hayo ya Copy
Cat Afrika Mashariki.
“kampuni
ya BMTL ilikuwa ni miongoni mwa kampuni ya Copy Cat kwa hiyo viongozi
wamekutana wa Afrika Mashariki wameona ni fursa ya kipekee kuunganisha
au kutumia jina moja la kibiashara (Brand) katika kujiimarisha katika
biashara za kompyuta na ufundi na utengenezaji wa mifumo ya mitandao na
mawasiliano nchini,” amesema Bw, Holtham
Amesema
kuwa kubadilisha jina la kibiashara na jambo la kawaida katika mkakati
wa kujiimarisha kibishara na kimasoko katika juhudi za kutafuta wateja
wapya na kupanua wigo wa biashara ili kukuza mauzo ya ndani na nje ya
nchi.

Afisa Mtendaji Mkuu, Bw Mike Holtham na akiwa pamoja na Mkuu wa Mauzo, Bw Avais Ansari wakizungumza na waandishi wa habari kwenye sherehe hizo zilizofanyika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar hivi karibuni.
Bw.
Holtham aliongeza kuwa kwa zaidi ya miaka 2o kampuni ya BMTL ilikuwa
chini ya kampuni ya Copy Cat na imewakilisha vizuri katika soko la
Tanzania kwenye maswala ya teknolojia na kompyuta.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mauzo, BMTL, Copy Cat, Avais Ansari amesema kuwa
kwa zaidi ya miaka 50 kampuni hiyo imejikita kwenye maswala ya ulinzi wa
kutumia teknolojia na uchapaji wa vitu mbalimbali kwa kutumia kompyuta
hapa nchini.
“kubadilisha
jina na kwenda kwenye kampuni mama ya Copy Cat ni mkakati tu kwa
kibiashara katika jitihada ya kukuza na kupanua biashara zetu hapa
Tanzania,” amesema Bw, Ansari
Amesema
kampuni hiyo ipo pia katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia na
Tanzania na wana mkakati wa kwenda nchi zingine kusini mwa jangwa la
sahara.



No comments: