Ilikuwa Mida ya Saa tatu za asubuhi ambapo Magari zaidi ya 10 ya Jiji yalikuwa yamejipanga eneo la mwenge Huku kukiwa na Ma Askari wa FFU wa kutosha pamoja na Migambo wa Jiji huku wakiongozwa na watu wa Jiji kwa ajili ya Kukamilisha swala zima la bomoa bomoa vibanda vyote ambavyo havina mpangilio, zoezi
hilo lilianza kwa utulivu na kuendelea kwa utulivu kutokana na ulinzi mkubwa uliokuwepo huku wananchi wakiendelea na kazi zao kama kawaida na kukatazwa kukatiza katika eneo la tukio kwa usalama wao.
Hata hivyo Baada ya vibanda hivyo kutolewa kumegundulika kuwa kulikuwa ni kuchafu kupindukia kutokana na uchafu uliokuwa umezagaa kila kona.
Kulia ni Magari mbalimbali ya Serikali yakiwa yamepaki eneo la Mwenge huku zoezi likiendelea
BOMOA BOMOA YA VIBANDA VYA BIASHARA MWENGE
Huwezi amini lakini ndio hali halisi sasa eneo jirani na Kituo cha Mabasi Mwenge hakuna tena Adha ya vibanda , lakini umebaki uchafu uliopitiliza na kugundulika kuwa hawa watu walikuwa wakifanya Biashara katika maeneo ambayo si salama
Hili ni eneo ambalo lilikuwa ni Maarufu kwa ajili ya kuuza vitu mbalimbali kama mitumba na viatu lakini kwa sasa hakuna kitu ni peupe
Huu ni uchafu uliopitiliza
Kwa wale akina dada hili lilikuwa eneo maarufu sana kwa ajili ya Kutengenezea nywele na saloon bubu ambazo zote zimevunjwa vunjwa kwa sasa
Hapa juu mwanzo kulikuwa na mabanzi ya kutosha na wakina dada wengi walikuwa wanapenda kuwa hapa wakitengenezwa nywele zao wasijue kuwa walikuwa wakikaa katika eneo chafu kama hili.
Kwa kuliangalia Eneo hili utasema ni chafu sana lakini ndio ambalo lilikuwa maarufu hasa kwa akina mama na akina dada kutengenezea kucha zao na kusuguliwa miguu, Je kama wangejua ni pachafu hivi wangeweza kugusa hata kuja kutengeneza kucha?
Baada ya kufanya manunuzi watu hutupa takataka tuu, zilikuwa zikijificha kulingana na mkusanyiko wa watu lakini hii ndio hali halisi sasa
Huu ni upande wa pili wa kuelekea Mikochemi ambapo bajaji Hupaki napo wamesafisha kwa kubomoa vibanda vyote hapa ni Shwari peupe
Picha hizi mbili ni eneo maarufu sana ambapo watu walikuwa wanauza Vifaa vya umeme na DVD, Sub Woofer pamoja na Radio bila kusahau TV sasa pamebaki kama hivi, Je walikuwa hawajui kama ni pachafu kiasi hiki?

No comments: