Tuesday, July 15, 2025

ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5

                                

MAANDALIZI ya ujenzi wa kijiji cha michezo kitakachojulikana kama Jakaya Kikwete Sports Village yanaendelea vizuri, ambako tayari Ikulu, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Wizara ya Michezo wametoa baraka kijengwe mjini Dodoma.
Akizungumza na Tanzania Daima, Mratibu wa ujenzi wa kituo hicho, Wilhelm Gidabuday, alisema ujenzi wa kituo hicho kikubwa na cha kwanza nchini, tayari maandalizi yake yameshafikia pazuri na Ikulu ya Tanzania kupitia ofisi ya Katibu wa Rais, imeshawapa baraka ya kutumia jina la Rais katika kituo hicho.

Gidabuday alisema, wiki iliyopita walikutana na Katibu wa Rais, ambako waliwasilisha maombi yao na kukubaliwa na kwamba, kuanzia sasa kituo hicho ambacho ujenzi wake utasaidia kuinua vipaji vya michezo yote hapa nchini, kitafahamika kama kituo cha michezo cha Jakaya Kikwete (Jakaya Kikwete Sports Village).
“Nidokeze tu kuwa mipango yote inakwenda sawa tumeshafikisha ujumbe wetu Ikulu na imekubalika, awali tulipanga kituo chetu tukiite John Steven Akhwari Sports Village lakini baada ya kukaa na Mzee Akhwari, kwa pamoja tuliridhia kituo hiki kitumike kama sehemu ya kumpa heshima Rais wetu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete hivyo kitafahamika kama Jakaya Kikwete Sports Village” alisema Gidabuday.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
TAARIFA MAALUM YA IKULU KWA UMMA KUHUSU ZIARA YA RAIS UINGEREZA
»
Previous
RATIBA NBA USIKU WA KUAMKIA KESHO

No comments:

Post a Comment


Top