
Mkurugenzi wa Majisafi na Majitaka Sumbawanga (SUWASA), mkoani Rukwa,
Antipas Shirima akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu
Abdulrahman Kinana kuhusu ujenzi wa tanki la lita milioni moja za
majisafi linalojengwa katika mradi wa SUWASA unaotarajiwa kumalizika
Machi 7, mwakani (2015). Mradi huo mpaka unakamilika utagharimu kiasi
cha fedha shilingi Bilioni 30. Pamooja na kutembelea mradii wa maji safi pia alitembelea mradi wa maji taka wilayani humo, Ndugu Kinana anamaliza zaira yake leo ya siku sita mkoani Rukwa.

Sehemu ya eneo hilo ambapo litajengwa tanki la lita milioni moja za maji safi na kusambazwa Wilaya ya sumbawanga na vijiji mbalimbali mkoani Rukwa.

Mkurugenzi wa Majisafi na Majitaka Sumbawanga (SUWASA), mkoani Rukwa, Antipas Shirima akimuelekea jambo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuhusu ujenzi wa eneo la kisima cha kuchujia maji safi na hatimaye kuyapeleka kwenye matanki na baadaye kusambazwa sehemu mbalimbali za wananchi mkoani Rukwa.
No comments: