Mratibu wa Mradi wa Kupinga ukatili wa kijinsia na ukatili wa Watoto kutoka Kihumbe, Sonja Mnyani alisema lengo ni kuijulisha jamii kujua sera zinazohusu ukatili wa kijinsia na watoto.
Mgeni rasmi katika Kampeni hiyo, Violeth Mwakatuma ambaye pia ni Afisa Mtendaji wa kata ya Bulyaga alilipongeza shirika la Kihumbe kwa kampeni hizo na kusisitiza jamii kuacha vitendo hivyo.
Mh. A ugustine Lugome Hakimu makzi Mahakama ya Mwanzo Kandete akitoa mafunzo ya sera zinazopinga ukatili wa kijinsia
Rose Mbolio Mwenyekiti wa dawati la kupinga ukatili wa kijinzia wilaya ya Rungwe akitoa mada ya kuhusu ukatili wa kijinsia
Kikundi cha sanaa cha kihumbe kikionyesha umahili wake wa kucheza sarakasi
Baadhi ya wananchi wakiwa makini kusikiliza mafunzo hayo
Baadhi ya waelimisha jamii wakitoa mafunzo kwa wananchi
Mafunzo yanaendelea sokoni Tandale
Baadhi ya wananchi wakipata mafunzo na kupima afya zao
Kama kawaida watoto hawakuwa nyuma kusikiliza mafunzo hayo
Shirika la Huduma Majumbani Mkoa wa Mbeya(KIHUMBE) linalofadhiliwa na WRP Chini ya Shirika la HJFMRI la watu wa Marekani limeendesha kampeni kwa jamii kuhusu sera zinazopinga ukatili wa kijinsia.
Akizungumza wakati wa kufunga kampeni hiyo Mratibu wa Mradi wa Kupinga ukatili wa kijinsia na ukatili wa Watoto kutoka Kihumbe, Sonja Mnyani uliofanyika katika kata ya Bulyaga wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya hivi karibuni alisema lengo ni kuijulisha jamii kujua sera zinazohusu ukatili wa kijinsia na watoto.
Alisema Kampeni hiyo ililenga kuelimisha jamii kuhusu sera zinazopinga ukatili wa kijinsia ili jamii ielewe haki zao za msingi na maeneo wanayopaswa kukimbilia kupata msaada baada ya kukumbwa na ukatili wa aina yoyote.
Alisema kampeni hiyo ililenga katika Kata tano za Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ambazo ni kata za Bagamoyo, Bulyaga, Malindo, Masoko na Mpuguso pamoja na kata moja katika Halmashauri ya Busokelo ambayo ni kata ya Kambasegera.
Aliongeza kuwa Wanawake wengi pamoja na watoto ndiyo wanaoathirika na ukatili wa kijinsia kutokana na maumbile yao ingawa pia kuna wanaume wanaofanyiwa hivyo lakini wanashindwa kutoa taarifa.
Mratibu huyo aliongeza kuwa zoezi hilo limelenga jinsi zote ili kuwakumbusha wanajamii kuchukua hatua za haraka pindi wanapokumbwa na ukatili ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wanaume na wanawake kuacha ukatili dhidi ya wenzie.
Alisema hakuna mfumo maalumu unaomwelekeza mwathirika wa ukatili kwa kukimbilia ingawa kuna vituo vingi vikiwemo dawati la Jinsia katika vituo vya Polisi, ofisi za ustawi wa jamii katika ngazi za kata na Watendaji wa Kata.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika Kampeni hiyo, Violeth Mwakatuma ambaye pia ni Afisa Mtendaji wa kata ya Bulyaga alilipongeza shirika la Kihumbe kwa kampeni hizo na kusisitiza jamii kuacha vitendo hivyo.
Aliongeza kuwa ni vyema wanajamii kutokaa na matukio hayo majumbani kwao bali wanapaswa kutoa taarifa katika vyombo vya sheria ili wahusika wachukuliwe hatua inayostahili.
No comments: