
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete (aliyenyoosha
mkono), akimuonyesha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana mandahari ya
eneo la Ziwa Tanganyika, linalotumiwa na wavuvi katika eneo la Kabwe
wilayani Nkasi mkoani humo, Kinana alipokuwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia ya kuzitatua katika eneo hilo la Wavuvi.

Katibu Mkuu wa CCM akitazama eneo la uvuvi katika ziawa Tanganyika, kwenye eneo la Kabwe mkoani Rukwa

Mfanyabiashara ya kusafirisha na kusindika samaki kutoka ziwa Tanganyika, Mohamed Shibibi (wapili kushoto) akimpatia maelezo Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana jinsi anavyohifadhi samaki katika majokofu baada ya kuvuliwa, Kinana alipokagua shughuli za mfanyabiashara huyo, kwenye eneo la wavuvi wa Kata ya Kabwe, wilayani Kansi mkoani Rukwa leo. Kushoto ni Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume.

Mfanyabiashara ya samaki Abuu Kitandu, akimuonyesha Kinana ukaushaji wa samaki kwenye kituo cha wavuvi cha Kabwe, wilayani Nkasi mkoani Rukwa

Kinana akitazama lundo la samaki aina ya migebuka kwenye kituo cha wavuvi cha Kabwe, katika ziwa Tanganyika

Mkazi wa Kabwe wilayani Nkasi mkoani Rukwa akiwa na mzigo wa migebuka aliowanunua kwa wavuvi katika ziwa Tanganyika

Mtoto Khalifa Saidi (5) akiwa amebeba samaki kwenye eneo la wavuvi la Kabwe, wilayani Nkasi

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wajengo la Ofisi ya CCM Kata ya Kabwe, mkoani Rukwa.

Wananchi wa Kabwe, wakiwa wamebeba samaki mkubwa kutoka Ziwa Tanganyika, wakati Kinana na Mbunge wa Nkasi Kaskazini Ali Kessy wakiwafuata kwa nyumba baada ya kutoka kukagua shughuli za wavuvi katika eneo lawafugaji la Kabwe mkoani Rukwa.


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi kwenye Ofisi ya CCM Kata ya Kabwe, wilayani Nkasi mkoani Rukwa leo.

Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume, akihutubia wananchi katika mkutano wa Kinana, uliofanyika leo kwenye Ofisi ya CCM Kata ya Kabwe leo.


No comments: