MABAO mawili ya
penalti ya Steven Gerrard yameipa ushindi wa 2-1 Liverpool na kuweka hai
matumaini ya ubingwa wa Ligi Kuu ya England.
Lakini timu zote, West
Ham na Liverpool ziliondoka uwanjani zimemkasirikia refa Anthony Taylor kwa
kuvurnda katika maamuzi yake kwenye mchezo huo ambayo yaliiponza timu kufungwa
bao.
West Ham walilalaimia
penalti iliyotolewa kabla ya mapumziko baada ya James Tomkins kuunawa mpira na
Gerrard akafunga dakika ya 44. Lakini wachezani waLiverpool walilalamikia pia
bao la kusawazisha la West Ham lililofungwa Guy Demel dakika ya 45.
Mshambuliaji wa zamani
wa Wekundu hao wa Anfiled, Andy Carroll alimchezea rafu ya wazi na kipa Simon
Mignolet wakati wa mpira wa kona, akimpiga kichwani na kusababisha Mbelgiji
huyo mpira umponyoke na kuangukia kwa Guy Demel, aliyefunga akiwa anatazamana
na nyavu.
Liverpool ilipata bao
la pili kwa penalti ya utata, baada ya kipa wa West Ham, Adrian kudaiwa
amemchezea rafu Jon Flanagan, lakini picha za marudio ya Televisheni
zilimuonyesha mlinda mlando huyo akiufikia mpira kwanza na Gerrard akaenda
kufunga.
Ushindi huo unaifanya
Liverpool ifikishe pointi 74 baada ya kucheza mechi 33 na kuendelea kula raha
kileleni mwa Ligi Kuu ya England, mbele ya Chelsea yenye pointi 72 za mechi 33
na Manchester City yenye pointi 70 za mechi 31.
No comments: