Klabu ya Manchester United imeambulia sare ya 1-1 dhidi ya mabingwa watetezi, Bayern Munich katika nusu fainali ya kwanza. Hadi mapumziko hakuna aliyeona lango la mwenzake licha ya kosa kosa za hapa na pale.
Cha pili Moyes alifanya mabadiliko yakuwatoa Giggs na Buttner na nafasi zao kuchukuliwa Kagawa na Young, Bayern akicheza kwa kujiamini na kutawala kiasi kikubwa cha mchezo huku Man U kutumia mashambulizi ya kushtukiza.
Mabadiliko hayo yalizaa matundu baada dakika ya 56 Vidic kufunga kwa kichwa kupitia mpira wa kona. Bayern nao wakafanaya mabadiliko yakuwatoa Muller na Kroos nafasi zao zikachukuliwa Mandzukic na Gotze.
Dakika ya 71 Bayern walisawazisha kupitia Shweinsteiger kwa kumalizia pasi ya kichwa toka kwa Mandzukic. Shweinsteiger alionyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kumfanyia madhambi Rooney na kulazimika refa kumtoa nje kwa kadi nyekundu.





Hadi filimbi ya mwisho ya Muamuzi inalia Ma U 1 Bayern Munich 1, wiki mbili mbele watarudiana kwa mechi ya pili nchini Ujerumani.
No comments: