Mkuu
wa Wilaya wa Songea Mjini Joseph Mkirikiti akikata utepe kuashiria
ufunguzi wa duka jipya la Tigo lililopo mjini Songea mtaa wa Shafi Bora
asubuhi ya leo mkoani Ruvuma. Wakishuhudia kutoka kushoto ni Meneja wa
Mauzo wa Tigo wa mkoa wa Ruvuma Kelvin Mibazi na Meneja wa duka hilo
kutoka Tigo Wilfred Nestory.

Mkuu
wa Wilaya wa Songea Mjini Joseph Mkirikiti (kulia) akifurahia zawadi ya
kadi ya kipaumbele aliyozawadiwa mapema leo na Mtaalam wa Huduma kwa
Wateja kutoka Tigo Jackson Jerry. Kadi hiyo inampatia mteja wa Tigo
huduma za kipekee kama kutokukaa katika foleni anapofika katika duka la
Tigo pamoja na kuondelewa kwa gharama mbali mbali anapohudumiwa katika
maduka hayo.

Mtaalam
wa Huduma kwa Wateja kutoka Tigo Jackson Jerry (kulia) akimuelezea Mkuu
wa Wilaya ya Songea Mjini Joseph Mkirikiti mapema leo kuhusu huduma ya
Tigo Pesa inayopatikana katika duka hilo. Akishuhudia kushoto ni Meneja
wa Mauzo wa Tigo kwa mkoa wa Ruvuma Kelvin Mibazi.

Mkuu
wa Wilaya wa Songea Mjini Joseph Mkirikiti akizungumza na wakazi na
wateja wa Tigo kutoka Songea mjini (hawapo pichani) mapema leo. Mkuu
huyo wa Wilaya aliipongeza Tigo kwa hatua hiyo ya kusogeza karibu huduma
zake pamoja na kutoa ajira kwa vijana wa mkoani Ruvuma kupitia duka
hilo.

Baadhi
ya wateja waliohudhuria hafla fupi ya uzinduzi wa duka hilo la Tigo
linalopatikana mtaa wa Shafi Bora Songea mjini wakimsikiliza Mkuu wa
Wilaya Joseph Mkirikiti alipofika kuzindua duka hilo.

Mkuu
wa Wilaya ya Songea Mjini Joseph Mkirikiti (mwenye suti) katika picha
ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya simu Tigo wa mjini Songea.

Mtaalam
wa Huduma kwa Wateja kutoka Tigo Jackson Jerry (kushoto) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu huduma mbali mbali
zitakazotolewa na duka jipya la Tigo lililopo Songea mjini. Huduma hizo
ni kama kuunganishwa kwa intaneti, kusajili na kupata upya laini, kuuza
simu za kisasa, Tigo Pesa n.k. Akisikiliza kulia ni Meneja Mauzo wa Tigo
kwa mkoa wa Ruvuma Kelvin Mibazi.
Tigo
leo imefungua duka jipya la huduma kwa wateja mjini Songea ambayo
itarahisisha upatikanaji wa huduma zake kwa wateja wa mjini hapo ambao
awali walikuwa hawana namna ya kupata huduma za moja kwa moja kutoka
kwenye kampuni hiyo ya simu.
Uzinduzi
huo umehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya wa Songea Mjini Bw. Joseph
Mkirikiti, ambaye ameipongeza Tigo kwa hatua yake ya kuzidi kusogeza
karibu huduma zake kwa watu wa Songea.
“Pamoja
na utatuzi wa kero za mawasiliano naamini ya kwamba duka hili jipya
litakuwa kama kituo cha kutoa huduma mbali mbali ambazo wateja wenu wa
Songea watakuwa wanahitaji kutoka kwenu kila siku,” alisema Mkirikiti.
Bw.
Mkirikiti alisema kwamba huduma mbalimbali za mawasiliano zitolewazo na
kampuni ya simu ya Tigo kama vile kupiga simu, kutuma SMS, mtandao wa
Intaneti pamoja na huduma ya kutuma na kupokea fedha, zimekuwa kichocheo
kikubwa katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini. “Aidha
huduma hizi zimeleta mageuzi chanya katika ufanyaji biashara na kuinua
hali ya maisha ya maelfu ya Wanasongea na mamilioni ya watanzania kwa
ujumla,” alisema.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini Bw. Jackson
Kiswaga, amesema tawi hilo ambalo linalopatikana Songea mjini mtaa wa
Shafi Bora linatarajia kuwahudumia wateja wapatao 150 kwa siku kwa
kuwapa huduma mbali mbali za Tigo zikiwemo huduma ya kuunganishiwa
intaneti, usajili wa laini za simu, Tigo Pesa na huduma maalum za simu
za kisasa (“Smartphones”).
“Duka
hili lina manufaa makubwa kwa wateja kwa sababu limeleta huduma zetu
karibu zaidi kwao. Pia linapatikana sehemu nzuri kibiashara kiasi kwamba
litavutia hata wateja kutoka wilaya zingine na maeneo jirani kama
Mbinga, Namtumbo, Tunduru Songea vijijini na Nyasa,”alisema Kiswaga.
Duka
hili linatoa huduma nyingine maalum zikiwemo uuzaji wa bidhaa mbali
mbali kama simu za kisasa ambapo mteja anaruhusiwa kuzijaribisha kabla
ya kununua. “Hii inamuwezesha mteja kufanya uamuzi sahihi katika
kuchagua na kununua bidhaa inayokidhi mahitaji yake.”
Tawi
la Songea linafikisha jumla ya maduka yanayoendeshwa na kampuni ya Tigo
nchini kufikia 40. Kwa mujibu wa Kiswaga, kampuni hiyo ina mipango ya
kufungua maduka mengine mengi zaidi katika sehemu mbali mbali nchini.
No comments: