Vijiji 1,400 vina Mipango ya matumizi bora ya ardhi kati ya zaidi ya 14,000 vilivyopo nchini hali inayochangia kuongezeka kwa migogoro ya ardhi kati ya hifadhi za taifa na wananchi, wakulima na wafugaji na wawekezaji na wananchui.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hii, Afisa Mipango Bora ya Ardhi kutoka Tume ya Mipango ya matumizi Bora ya ardhi, Jerome Nchimbi alisema hiyo ni changamoto kubwa na inayotakiwa kupatiwa ufumbuzi wa haraka.
Alisema kila kijiji nchini kinatakiwa kuwa na mpango huo unaoeleza juu ya matumizi ya ardhi kwa ajili ya dhughuli mbalimbali ikiwemo kilimo, malisho ya mifugo, makazi na hifadhi.
Naye Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa wa Iringa, Adam Swai alisema kati ya vijiji 361 vilivyopo ni vijiji 121 vimekamilisha mipango ya matumizi bora ya ardhi hali inayosababisha kutokuwa na migogoro isiyo ya lazima.
"Tukifanikiwa kupata mipango bora ya matumizi bora ya ardhi basi hatutakuwa na migogoro ya kati ya wakulima na wafugaji, hifadhi za taifa na wananchi, wanyama na binafamu na wananchi na wawekezaji", alisema Swai
Alisema watendaji wa Halmashauri na wadau mbalimbali wanatakiwa kutoa msaada ili kuhakikisha kila kijiji kinafikia lengo la kuwa na mpango wake.
Naye Mratibu wa Mratibu wa Mradi wa Kuboresha Mtandao wa Maeneo ya Hifadhi Kusini mwa Tanzania (SPANEST) unaoendeshwa kwa pamoja kati ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Shirika la maendeleo la umoja wa mataifa (UNDP), Godwell Ole Meinng'ataki alisema wamefiakia hatua hiyo ili kupunguza kwa kiwango kikubwa migogoro iliyopo kati ya vijiji vinavyozunguka hifadhi na hifadhi zenyewe.
Alisema ni tatizo kubwa kwa vijiji hasa vile zinavyozunguka hifadhi za Taifa kutokana na mwingiliano wa wanyama na pia wananchi kutoelewa matumizi mazuri.
Naye Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili wa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Juliana Pilla alisema dawa ya kuondoa migogoro ya ardhi vijijini na kila kijiji kuwa na Mpango wa matumizi bora ya matumizi ya ardhi. Alisema lakini kinachotokea ni kuwa vijiji vichache vina mipango hiyo jambo ambao linahitaji nguvu ya pamoja ya wadau wote ili kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi.

No comments: