ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5


 Mfanyakazi wa kampuni ya Fusun Investment Co. United akifanyakazi katika moja ya mashine zinazotumika katika usagaji wa chupa chakavu za plastiki kabla ya kusafirishwa nchi za nje. Kampuni hiyo imetoa ajira zaidi ya 300 tangu ilipoanzishwa mwaka 2010, na inampango wa kujitanua katika mikoa mingine Tanzania.
 Mfanyakazi wa kampuni ya Fusun Investment Co. United Limited akikusanya chupa chakavu za plastiki kwa ajili ya kuzisaga. Zaidi ya watanzania 300 wanafanyakazi katika kampuni hiyo ya kichina ambayo ukusanya chupa chakavu zaidi ya tani 700 kwa mwezi. Kampuni hiyo imesema inampango  wa kujitanua katika mikoa mingine Tanzania.
 Lundo la chupa chakavu za plastiki zikisubiria kusagwasagwa na kiwanda cha Fusun Investment Co. United Limited kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam. Kampuni hiyo ya kichina ukusanya chupa chakavu zaidi ya tani 700 kwa mwezi, na kwa sasa inampango wa kujitanua katika mikoa mingine Tanzania.
Lori lililobeba chupa chakavu za plastiki likiwa tayari kushusha chupa hizo kwa ajili ya kusagwa katika kiwanda cha Fusun Investment Co. United Limited kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam. Kampuni hiyo ya kichina ukusanya chupa chakavu zaidi ya tani 700 kwa mwezi, na kwa sasa inampango  wa kujitanua katika mikoa mingine Tanzania.

KAMPUNI ya kuhuisha (recycling) plastiki ya kichina inayofanya shughuli zake jijini Dar es Salaam ina mpango wa kutanua shughuli zake kwa kuwekeza zaidi nchini na kuongeza ajira zaidi kwa watanzania.

Kampuni hiyo, Fusun Investment Co. United Limited imesema jijini Dar es Salaam jana wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika kiwanda cha kampuni hiyo kilichopo Kurasini, kuwa ajira zaidi ya 300 zimeshatolewa mpaka sasa.

 “Wakati biashara yetu ikiendelea kutanuka, kuna uwezekano mkubwa wa sisi kuweza kuajiri watu wengi zaidi,” alisema Bw. Jiang Jiaxing, Mkurugenzi wa kampuni hiyo.

Alisema kuwa kampuni hiyo iliyoanzishwa tangu Desemba mwaka 2010 inakusanya tani 700 ya chupa za plastiki toka mtaani kwa wananchi kila mwezi na kuzisaga kuwa chakavu na kuzisafirisha nchini China kwa ajili ya kutengeneza vifaa vya plastiki vipya.

Pia, alisema kuwa kampuni yake imefungua viwanda viwili vilivyopo katika maeneo ya Mabibo na Mikocheni jijini Dar es Salaam na mipango zaidi inafanyika ya kujitanua shughuli zake zaidi katika mikoa mingine vijijini.

“Tumechangia katika uchumi wa Tanzania kwa njia nyingi kama vile kuingizia nchini fedha za kigeni, mapato kwa njia ya malipo ya kodi na ushuru pamoja na kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira kwa kukusanya plastiki zinazo zagaa ovyo kisha kuhuisha,” alisema na kuongeza:

“Hebu tafakari, nini kingeweza kutokea endapo tani 700 za chupa chakavu za plastiki zingeachwa zikizagaa mitaani?. Ingelikuwa ni tatizo kubwa”.

Ripoti za hivi karibuni zinaonyesha kuwa Dar es Salaam inakumbwa na tatizo kubwa la utunzaji wa takataka ngumu. Ikiwa ni jiji la tatu linalokua kwa kasi katika nchi za Jangwa la Sahara na la tisa duniani, linakumbana na changamoto kubwa ya jinsi gani ya kutunza taka zinazozalishwa. 

Tafiti zilizofanyika katika miaka ya 1980 zilionyesha kuwa jiji la Dar es Salaam linazalisha zaidi ya tani 1,200 ya taka ngumu kila siku, lakini tafiti za hivi karibuni zinaonyesha taka zizalishwazo jijini kwa sasa zimeongeza kwa zaidi ya tani 2,500 kwa siku. Jiji halina miundombinu ya kutosha inayohitajika katika kushughulikia ongezeko la taka ngumu na wingi wa taka maji zilizopo.

Tatizo la utunzaji taka la jijini Dar es Salaam linalenga zaidi utupaji wa taka na usafi wa mazingira, takataka zisizokusanywa zikiachwa zimezagaa mitaani,au kuchomwa moto kiholela katika kona mbali mbali za mitaa.

Changamoto hasa ni katika maeneo ya mijini ambayo yamekuwa yakiongezeka zaidi katika miaka michache iliyopita. Kumbukumbu zinaonyesha kuwa kati ya mwaka 1965, miaka michache baada ya uhuru na leo idadi ya wakazi wa mijini nchini Tanzania imeongezeka kutoka asilimia 5.0 mpaka zaidi ya asilimia 36 kwa sasa. Mlipuko huu wa ukuaji wa miji hauendani na uwezo wa kuzikabili taka zinazozalishwa.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top