MAJUKUMU YA KAZI
Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha
Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori
Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali
Kufanya usafi naulinzi wa kambi
Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao kwenye hifadhi
Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na kukusanya takwimu zao
Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na nyara nje na ndani ya Nchi
Kudhibiti wanyamapori waharibifu
Kudhibiti moto kwenye hifadhi
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Astashahada ya
Uhifadhi Wanyamapori (Technician Certificate in Wildlife Management)
kutoka Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi au chuo kingine
kinachotambuliwa na Serikali.
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B2 kwa mwezi.
MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA III – (NAFASI 327)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
MAJUKUMU YA KAZI
Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha
Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori
Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali
Kufanya usafi na ulinzi wa kambi
Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao kwenye hifadhi
Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani
Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na kukusanya takwimu zao
Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na nyara nje na ndani ya Nchi
Kudhibiti wanyamapori waharibifu
Kudhibiti moto kwenye hifadhi
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Astashahada ya Awali
ya Uhifadhi wa Wanyamapori (Basic Technician Certificate in Wildlife
Management) kutoka Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi au chuo
kingine kinachotambuliwa na Serikali.
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B1 kwa mwezi.
No comments: