ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5


Ilipoishia Mzee Joseph akamuambia Maria "Binti umependeza sana we mrembo kweli Johnson anajua kuchagua" Maria akacheka kusikia vile
Endelea Mzee Joseph alizidisha kumsifia Maria akamuambia "yani binti Mungu amekupa kila kitu ambacho mwanamke anatakiwa awe nacho ndio maana Johnson hataki kukuacha."
Maria: "mbona mimi wa kawaida tu mzee wapo wanawake wazuri warembo sio mimi Johson wangu ananipenda tu kutoka moyoni."
Mda wote huo mzee Joseph anaongea na Miria yeye Johnson alikuwa anawasikiliza tu huku anatabasamu.
Mzee Joseph: "lakini sasa binti naomba kuna kitu nikuulize sijui kama uko tayari?
Maria: "uliza tu mzee wangu wala usijali"
Mzee Joseph: "msichana mzuri mrembo kama wewe unatokea familia ya kitajiri kama ile kweli unakubali mpenzi wako awe rafu hivyo awe anateseka kuuza genge?
Maria akaguna kusikia lile swali akamjibu "mimi sipendi mzee ila sasa si ndio kazi yake aliyoichagua tangu muda mrefu anaifanya mimi siwezi kumzuia sababu ndio kazi inayomfanya aishi na mimi Johnson nampenda sana hivyo hivyo alivyo na kazi yake."
Mzee Joseph: "wewe huoni hata aibu rafiki zako wakijua unatembea na muuza genge au bahati mbaya siku wakukute hapa upo na Johnson yupo hivyo hutajisikia aibu?
Maria: "mimi sijali mzee hata siku Johnson awe chizi mimi nitampenda na kumuheshimu sababu ndio mwanaume wa maisha yangu niliyemchagua na ndio mwanaume pekee anayeujua mwili wangu nimetoka naye mbali sana"
Johnson akawa anawasikiliza tu huku anacheka cheka alikuwa anataka aone mwisho wa yale maongezi utakuwaje.
Mzee Joseph: "binti nimekusifu nimeyapenda sana majibu yako lakini kuna kitu nataka nikuambie kama kweli unampenda huyu kijana fanya uwe unamsaidia wewe wazazi wako ni matajiri sana ni watu maarufu sana hapa mjini najua lazima na wewe pesa kwako sio tatizo sababu umezaliwa peke yako wewe ukipata pesa jitahidi uwe unamsaidia mpenzi wako aongezee hata mtaji aache kazi ya kuuza genge siku moja, handsome kama huyu hii kazi haimfai anafanya basi tu sababu pesa hakuna."
Johnson akainama akawa anasubiri kusikia jibu kutoka kwa Maria.
Maria: "kweli mzee mimi kwetu tuna uwezo na wazazi wangu nikitaka chochote kile wananipa lakini huyu Johnson muoga sana nakumbuka wakati tunasoma naye nilikuwa nikimununulia zawadi kubwa au nikimpa pesa alikuwa anaogopa kuzichukua ananiuliza mara mbilimbili nimezitoa wapi alikuwa ana wasiwasi kuwa nimewaibia wazazi wangu watakuja kumkamata hata siku hizi nikimnunuliaga vitu naonaga kama ana wasiwasi navyo ndio maana na mimi nashindwaga kumpa baadhi ya vitu hata nikiwa na pesa naonaga nikimpa ataanza kuniuliza maswali mengi na hajawahi kuniambia kuwa ana shida"
Mzee Joseph: "kweli binti lazima wasiwasi uwepo sababu Johnson alikuwa anajua kabisa wewe ni mwanafunzi mwenzake hufanyi kazi akawa anajiuliza unatoa wapi pesa za kumnunulia zawadi lakini zile zilikuwa akili za kitoto sasa hivi wote mmekua na Johnson ameshajua maisha yanavyoenda fanya kumsaidia mpenzi wako atoke kimaisha we unadhani atauza Genge hapa hadi lini."
Maria akamuangalia Johnson wote wakacheka Maria akamuambia mzee mbona sasa yeye haongei unamuongelea wewe mzee na yeye aongee nimsikie au ananionea aibu?
Johnson: "mimi nimemuachia kwanza mzee akuambie alafu mimi ndio nitamaliza kila kitu mimi na wewe haya mambo tutaongea vizuri tukiwa chumbani wawili msikilize kwanza mzee Joseph akupe somo"
Wote wakacheka Maria akamuambia Johnson "mimi mzee Joseph nimeshamuelewa sasa hili swala ungeliongea tangu muda sasa hivi si ungekuwa mbali sana mara nyingi wazazi wangu wananipa pesa mimi nazichezea kumbe wewe unataka uongezewe mtaji halafu husemi au unanidharau unaniona mimi sina pesa ya kukusaidia mimi nakupenda sana Johnson nitafanya juu chini hadi na wewe uwe na maisha mazuri"
Johnson alifurahi sana kusikia vile wakaangaliana na mzee Joseph wote wakatabasamu. Johnson: "sio kwamba mimi nakudharau mpenzi wangu mimi najua kabisa nyie kwenu ni matajiri sana nilikuwa naogopa kukuambia hili swala sababu nawaogopa sana wazazi wako na pia mimi nina aibu sana ya kumuomba mwanamke pesa ila kwa sasa naona muda unaenda na maisha yangu yapo vile vile na ukiangalia ndugu zangu wote wananiangalia mimi ndio maana nimeona nikuambie mpenzi wangu unisaidie chochote ulichonacho ili niweze kusonga"
Mzee Joseph: "wewe Johnson huujui ule msemo wa uoga wako ndio umasikini wako huyu binti mimi nimemuona hana tatizo anakupenda sana na ana lengo la kukusaidia anapenda sana uwe na maisha mazuri ila ameshajua wewe unaogopaga kupokea vitu anavyokupa ndio maana hata yeye kakukaushia wewe kaa naye chini vizuri muongee atakusaidia tu wewe si ndio chaguo lake"
Maria: "kweli mzee mimi Johnson nampenda sana na yeye pia anajua sasa nashangaa hata kama ana shida hatakagi kuniambia anaogopa wakati mimi sipendi kumuona anapata shida wakati mimi nipo hata kama ninacho kidogo kama yeye ana shida nitamsaidia tu kama sina tunakaa tunashauriana tufanye nini hivyo ndio inavyotakiwa"
Mzee Joseph akamshika Maria mkono akamuambia "wewe binti una akili sana nimeyapenda sana maneno yako hapo lazima kashakuelewa nitafurahi sana nikiona mnasaidiana na ninawaombea mzidi kupendana milele na milele"
Walivyomaliza maongezi yao Maria akawaambia "mimi ngoja niwahi nyumbani naona muda umeenda sana Baba na Mama wasije wakarudi wakanikosa na hilo swala la Johnson ngoja nikaanze kulifanyia kazi muda si mrefu nitampa jibu." Maria palepale akafungua pochi yake akatoa Elfu thelasini akampa Mzee Joseph Elfu kumi na Johnson akampa Elfu ishirini akawaambia zile ni pesa za kula amewapa Mzee Joseph alifurahi sana alimshukuru sana Maria. Johnson alimshika Maria kiuno wakaongozana hadi Bajaji zinapopaki Maria akapanda akaondoka zake

Itaendelea...................

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top