Ilipoishia
Maria alimpigia Johnson simu akamwambia anataka akalale
tena nyumbani kwake Johnson akamgomea akamwambia asije sababu wazazi wake
wanaweza wakarudi muda wowote
Endelea
Maria walibishana sana na Johnson Maria msimamo wake ulikuwa ni ule ule lazima akalale tena kwa Johnson sababu wazazi wake walimuambia kuwa watarudi kesho yake jioni Johnson hakuwa muongeaji sana alivyoona Maria anaendelea kung'ang'ania aje kulala nyumbani kwake akamkatia simu akaendelea na shughuli zake za pale gengeni huku akiwa na mawazo sana. Akaona haitoshi akamfuata mzee Joseph ili ampe ushauri akamuambia "mzee mimi yule binti bado ananichanganya muda huu tena kanipigia simu ananiambia leo tena anakuja kulala nyumbani kwangu wakati wazazi wake hawaeleweki watarudi mda gani" Mzee Joseph akamuambia "kijana yule binti anafanya yote hayo sababu tu anakupenda wewe fikiria anaacha kulala nyumbani kwao kwenye kila kitu anang'ang'ania kuja kulala kwenye kagheto kako muuza genge. Kusikia vile ikabidi Johnson acheke tu mzee Joseph alikuwa ni mtu wa utani mwingi sana ndio maana vijana wengi walitokea kumpenda Johnon akamuambia "mzee tuache utani mimi nimekuja kwako kuomba ushauri nifanyaje usije siku ukasikia kijana wako nipo segerea" yule mzee akacheka akamuambia "Yani we kijana inaonyesha yule binti unamkuna vizuri sana unampa mambo mazuri mbona kakuganda sana jana tu umetoka kulala naye leo anataka tena cha kufanya hapo awapigie simu wazazi wake awaulize wanarudi lini akishajua ndo aje ulale nae kwako" Johnson akamwambia "mzee kaniambia wazazi wake kawapigia simu wamemuambia wanarudi kesho jioni sasa mimi bado siamini sina uhakika wasije wakarudi ghafla wakute binti wao hayupo waje nyumbani kwangu wamkute yawe kama ya siku ile" Mzee akamuambia "usiogope kijana yeye si ndo kasema wanarudi kesho we mruhusu aje tu wazazi wake wakirudi atajua yeye afanyaje" Johnson akamwambia "sikiliza mzee tatizo ni moja wazazi wa yule binti wameshapajua mimi ninapoishi wanaweza wakarudi ghafla usiku wakute binti yao hajalala pale waje kwangu watufume tumelala" Mzee Joseph akamwambia "sasa hapo kijana wangu mimi sina kingine cha kukushauri fanya unavyojua wewe kama roho yako inasita mwambie asije" Johnson hakuwa na cha kuongea akamuaga mzee Joseph akaondoka huku akiwa mnyonge sana ilikuwa jioni imeshaingia hakuwa tena na mzuka wa kuendelea kukaa pale gengeni kwako Alifunga genge lake akaanza safari ya kurudi kwake akajua lazima tu atamkuta Maria kule kwake lakini alivyofika akafungua mlango wake hakumkuta Johnson alifurahi sana akajua yale maneno yake yamemuingia Maria ndio maana hajaja pale kwake Alifika akawasha moto wake akaanza kufanya maandalizi ya kupika wakati anaandaa mboga yake akasikia mlango unagongwa akajiuliza nani tena kaja kwake usiku ule alivyofungua mlango alikuwa ni Maria Johson alikosa raha kabisa hadi nguvu ya kupika ikamuisha akaa kitandani kwake akamuuliza Maria "we binti mbona hupendi sana kunisikiliza mpenzi wako ninachokuambia?? Maria akamjibu "sio hivyo mpenzi wangu mimi nakupenda sana Johnson ndio maana nafanya hivi wazazi wangu wakiwepo nyumbani mimi siwezi kuja hapa kwako sasa hivi hawapo ndio mda wetu wa kujiachia" Johnson akamwambia "wewe unachotaka mimi niuliwe au nikaozee jela hakuna kingine" Maria akamjibu "nani atakuua mpenzi wangu yani siku we ukifa na mimi nakufa siku ukipelekwa jela na mimi bora nifungwe" Johnson akamuambia "hayo yote unaongea sababu bado hayajatokea we ngoja yatokee" Maria akatoa mfuko akampa Johson akamwambia "acha kupika mpenzi wangu nimekununulia chips kuku hizo kula baby wangu " Johson akauchukua ule mfuko akatabasamu akamtania Maria akamuambia "siku nikiwa jela sijui kama utaniletea vyote hivi au utatafuta mpenzi mwingine"
Itaendelea...............
No comments: