Klabu ya Azam imeendeleza wimbi la ushindi baada
yakuwafunga Simba SC magoli 2-1. Hamis Mcha alikuwa wakwanza kuwapatia
bao wanalambalamba hao dakika ya 24, dakika za nyongeza wakundu wa
msimbazi kupitia Joseph Owino wakasawazisha goli hilo
.Hadi
kuelekea mapumziko Azam 1 Simba 1, kipindi cha pili kilianza kwa kasi
kwa timu zote mbele kwa kupokezana kushambulia lakini bahati
ikawaangukia Azam baada ya tik taka ya Kipre Tcheche kugonga mwamba na
kumkuta mfungaji John Bocco dakika ya 56.
Kwa matokeo hayo Azam
amezidi kukaa kileleni baada yakujikusanyia pointi 53 kwa michezo 23
aliyocheza akifuatiwa na mabingwa watetezi Yanga SC kwa pointi 46 kwa
michezo 22 aliyocheza.
Waamuzi wa mchezo wakijiandaa kuingia uwanjani kupasha moto misuli
Azam wakipasha misuli
Picha na Hamis Shaku
No comments: